WAISLAMU WAOMBEA AMANI UCHAGUZI MKUU

Ben Komba/Pwani-Tanzania/9/6/2015 1:58:44 PM

Waumini wa dini ya kiislam nchini  wamefanya ibada maalum ya kuombea amani kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani ambao unatarajiwa kufanyika  Oktoba 25   mwaka huu.

Mkuu wa wilaya ya Kibaha, BIBI.HALIMA KIHEMBA kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Pwani, amesema kuwa viongozi wa dini wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa kunakuwepo na hali ya amani kabla ya uchaguzi,wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi.

Mkuu huyo wa wilaya BI.KIHEMBA ameongeza kuwa serikali ina wajibu wa kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa utulivu,haki na amani, ingawa serikali yenyewe haiwezi bbila kuwashirikisha wadau ambao ni pamoja na viongozi wa dini katika kuwahimiza waumini wao kufuata sheria na taratibu zilizopo.

 Naye SHEIKH LIPAMBILA MUDHIHIR akielezea kuhusu uumbaji amesema kuwa Mungu akiombwa anasikiliza, ametoa mfano kuwa Mungu ameumba binadamu mwanaume na mwanamke, ameumba jua na mvua na mambo mengine chungu nzima akitaka binadamu wamuogope na kumtukuza.

Amewaasa wanadamu kujua kuwa kuna Mungu kwa hiyo kitendo cha baadhi yetu kupuuza ibada kutawagharimu binadamu siku ya amri kiama na amefananisha kuheshimiwa ni kama mkusanyiko huo kuomba amani na wakiwa hawaelewi maana nzima ya tukio hilo.

Kaimu Mufti wa Tanzania SHEIKH ABUBAKAR ZUBEIR amesema Watanzania inawabidi kitunza amani iliyopo kwa hali na mali na hasa kutokana kama amani itavurugika hatutakuwa na pakukimbilia toka maelfu ya majirani zetu wanamiminika nchini kutokana ukosefu wa amani katika nchi wananzotoka.
SHEIKH ZUBEIR amewaasa watanzania kuwa macho na watu ambao wakiona mambo hayaendi kama wanavyotaka wao uamua kuanzisha vurugu na kuwaacha wanawake,wazee na awatoto katika dhiki kubwa.

END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA