CHADEMA KIBAHA VIJIJINI YAJIDHATITI.


Ben Komba/Pwani-Tanzania/9/6/2015 2:35:57 PM
Chama cha demokrasia na maendele-CHADEMA-kimezindua rasmi kampeni yake ya ubunge katika Jimbo la uchaguzi Kibaha vijijini kwa kutangaza vipaumbele vinne vilivyopo katika ilani ya uchaguzi wa chama hicho.

Makamu wa mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, BW.SAID ISSA MOHAMED amesema kuwa mgawanyo wa ubunge kwa UKAWA ni kwamba katika Mkoa wa Pwani chama cha demokrasia kina nafasi ya ubunge tatu na CUF wa nafasi saba.

BW.MOHAMED ameongeza hatua yoyote ya mwanacha mwingine kutoka umoja wa UKAW kugombea sehemu ambayo imetengwa kwa ajili ya chama shirika kingine ni usaliti ambao amesema utafanyiwa kazi ili kupata ufumbuzi.

BW.MOHAMED amewataka wananchi wa Kibaha kutokubali kununuliwa na CCM, Katika uchaguzi mkuu ujao, ilihali hali ya mambo ikizidi kuwa mbaya kutokana na kukosekana utawala bora ambao u nathamini ustawi wa wananchi.

Akimtambulisha mgombea Ubunge wa CHADEMA, BI.EDITHA BABEIYA amewataka wapiga kura kumchagua yeye ili aende kuwawakilisha bungeni na hasa ikizingatiwa yeye amekuwa mmoja wa wanawake saba ambao wamebahatika kuteuliwa kugombea nafasi hiyo.

Mgombea mbunge wa CHADEMA,Kibaha vijijini BI.EDITHA BABEIYA amesema kuwa anataka kwenda bungeni kwenda kuwawakilisha wana wa Kibaha vijijini baada ya Chama kumpima kwa kumpeleka kwa wananchi ili waweze kumpima ingawa tayari yeye ni Mbunge wa viti maalum.

Akizungumzia kuhusu tuhuma zinadai yeye anahusika na ufisadi alipokuwa DAWASCO, Amebainisha kuwa yeye akiwa kama Meneja Biashara wa DAWASCO alijaribu kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wakubwa zake wakampuuza na matokeo yake yakawa upotevu mkubwa wa fedha na ameahidi kushughulikia suala hilo atakapopata nafasi hiyo, kwani ana taarifa za kutosha juu ya suala hilo.


END.  

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA