Posts

Showing posts from February, 2014

WANANCHI WAJITOLEA KUJENGA DARAJA KIBAHA.

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/09:54/22/2/2014 Serikali ya Mtaa wa Muheza katika halmashauri ya mji wa Kibaha kwa kushirikiana na wananchi imeamua kujenga daraja kwa njia ya kujitolea ili kupunguza kero wanazopata kipindi cha msimu wa mvua. Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Muheza BW. MOHAMED LINGOWICHE amesema wameamua kuchukua uamuzi kutokana na kero zinazowakabili kipindi cha mvua na kusababisha maisha ya wananchi kuwa hatarini. BW.LINGOWICHE ameongeza kuwa kinachosaidia katika ujenzi huo wa makaravati ni kutokana na wananchi wake kuwa wenye kuzingatia mambo na kumuelewa pale alipoitisha kikao cha wananchi kuwaelezea kusudio la wananchi kujitolea kujenga makaravati hayo. Amefafanua kuwa Mbunge wa Jimbo la Kibaha, BW.SYLVESTER KOKA ametoa shilingi laki sita na wananchi wakichangia shilingi laki 2, na kuwezesha kuchongwa kwa barabara hiyo inayounganisha mtaa huo. \Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Barabara Mtaa wa Muheza, BW. ASHRAF MMARI amesema mpaka sasa ujenzi wa

CCM WATAKIWA KUACHA KUUZA MANENO

Image
Ben Komba-Pwani/Tanzania/2/21/2014 1:59:27 AM Katika kuonyesha kuwa maendeleo yoyote yanaletwa na wananchi, Kata ya Misugusugu mjini Kibaha imefanikiwa kupata ofisi ya kata yenye hadhi ya juu kufuatia juhudi zilizofanywa na viongozi na wan anchi wa kata hiyo. Diwani wa Kata ya Misugusugu ambaye pia ni mwenyekiti Baraza la madiwani wa halmashauri ya mji wa Kibaha, BW. ABUDHADI MKOMAMBO amesema hayo wakati wa uzinduzi wa jengo la ofisi ya kata ya Misugusugu iliyogharimu jumla ya milioni 45. BW.MKOMAMBO amesema ofisi yake kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imefanikiwa kujenga ofisi ya kata ambayo ipo katika kiwango cha kisasa na hivyo kurahisisha utendaji kazi wa viongozi wa Kata hiyo. Mwenyekiti huyo wa baraza la halmashauri amebainisha mbali ya ujenzi wa ofisi hiyo ya Kata, kata yake imekuwa ikitekeleza miradi ya ujenzi wa ofisi za mitaa ambapo mpaka sasa wameshafanikiwa kukamilisha ofisi hizo kwa asilimia 90 katika mitaa 4 ya kata hiyo. Akifungua ofisi hi

WAUZA MANENO WAONYWA KIBAHA

Image
CCM KIBAHA MJINI YAONYA WAUZA MANENO Ben Komba/Pwani-Tanzania/17 February 2014/ Wanachama wa chama cha mapinduzi mjini Kibaha wametakiwa kutokuwa madalali wa kisiasa na kuzua makundi ambayo yanhatarisha uhai wa chama katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa mitaa na baadaye wa uchaguzi mkuu mwaka 2015. Mwenyekiti wa CCM Kibaha mjini, BW.MAULID BUNDALA ameyasema hayo wakati akifungu kikao ch a baraza la wazazi Kibaha mjini, ambapo amesema kumekuwa kwa baadhi ya wana CCM kupita huko na huko kutafuta watu wenye fedha na kuwashawishi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi. Mwenyekiti huyo wa CCM amebainisha kuwa cha kushangaza zaidi watu wanaowafuata wengi wao wanakuwa hawana uzoefu katika siasa, na huku wakiwaacha makada wazoefu katika kuwapendekeza katika kugombea nafasi mbalimbali kwa kuwa tu hawana fedha. Aidha ameongeza CCM imefikia mahali ina madalali wa kisiasa wanaoishi kwa kutegemea kufanya utapeli wa kisiasa, kwa kutumia nafasi yao kama wanachama wa

CCM KIBAHA MJINI YAONYA WAUZA MANENO

Ben Komba/Pwani-Tanzania/17 February 2014/ Wanachama wa chama cha mapinduzi mjini Kibaha wametakiwa kutokuwa madalali wa kisiasa na kuzua makundi ambayo yanhatarisha uhai wa chama katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa mitaa na baadaye wa uchaguzi mkuu mwaka 2015. Mwenyekiti wa CCM Kibaha mjini, BW.MAULID BUNDALA ameyasema hayo wakati akifungu kikao cha baraza la wazazi Kibaha mjini, ambapo amesema kumekuwa kwa baadhi ya wana CCM kupita huko na huko kutafuta watu wenye fedha na kuwashawishi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi. Mwenyekiti huyo wa CCM amebainisha kuwa cha kushangaza zaidi   watu wanaowafuata wengi wao wanakuwa hawana uzoefu katika siasa, na huku wakiwaacha makada wazoefu katika kuwapendekeza katika kugombea nafasi mbalimbali kwa kuwa tu hawana fedha. Aidha ameongeza CCM imefikia mahali ina madalali wa kisiasa wanaoishi kwa kutegemea kufanya utapeli wa kisiasa, kwa kutumia nafasi yao kama wanachama wa CCM kuuza maneno kwa lengo la kujipatia mka

CHADEMA YATISHA PWANI YAKANA UDINI.

Image
CHADEMA YAWASHA MOTO PWANI NA KUPINGA KUJIHUSISHA KWAO NA UDINI. Ben Komba/Pwani-Tanzania/02-02-2014/13:07 Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimehitimisha kampeni yake ya kujitangaza ya vuguvugu la mabadiliko, pamoja daima katika mkoa wa Pwani, mjini Kibaha kwa kuwahakikishia Watanzania kuwa wao sio Chama cha kidini na ni Chama cha kila Mtanzania mpenda mabadiliko chanya ya nchi. Makamu wa Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, BW.ISSA MOHAMED amesema suala la udini ni agenda ya Chama tawala kutokana na kutumia kauli mbiu hiyo kujaribu kudhoofisha upinzani kama ilivyokuwa kwa chama cha wananchi-CUF- kwa kukiita chama hicho kuwa ni cha kidini. Kwa kutumia propaganda ya ukanda walifanikiwa kuiporomosha CUF kwa kipindi hicho kwa kudai kuwa chama hicho ni chama cha Wapemba na walipoona kuwa haitoshi wakaanzisha propaganda kuwa chama hicho ni chama cha kidini na kufanikiwa kuwaweka pembeni katika mchakato wa kisiasa kuinganisha na mwanzo wake. BW.MOHAMED amewaambia wana Pwani wamekuwa

YPC YAPONGEZWA NA MKUU WA WILAYA-BIBI KIHEMBA

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/01-02-2014/12:39 Mkuu wa wilaya ya Kibaha BIBI.HALIMA KIHEMBA ameyapongeza mashirika yasiyo ya kiserikali kwa kufanya kazi zao za kusaidia serikali kutekeleza majukumu yake ya kila siku. BIBI KIHEMBA akifunga kikao kati ya wakuu wa idara na wakurugenzi wa halmashauri zote mbili za halmashauri ya mji na wilaya ya Kibaha na Taasisi isiyo ya kiserikali ya YOUTH PARTNERSHIP COUNTRYWIDE, amesema kuwa kwa   sasa shughuli za mashirika yasiyo ya kiserikali zimeanza kuzaa matunda. Akizungumzia masuala mbalimbali ambayo yaliibuka kufuatia mrejesho wa shughuli zilizotekelezwa na shirika lisilo la kiserikali la YPC, Kuhusiana na migogoro ya wakulima na wafugaji, BIBI.KIHEMBA amefafanua kwa kutoa mfano wa kijiji cha Gumba ambacho kina mgogoro mkubwa wa ardhi lakini watendaji wa kijiji na kata wanangojea Mkuu wa wilaya atoe tamko. Mkuu huyo wa wilaya BIBI.KIHEMBA ameongeza   sheria kuhusu matumizi bora ya ardhi yapo wazi na sheria zipo wazi laki