CHADEMA YATISHA PWANI YAKANA UDINI.

CHADEMA YAWASHA MOTO PWANI NA KUPINGA KUJIHUSISHA KWAO NA UDINI.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/02-02-2014/13:07
Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimehitimisha kampeni yake ya kujitangaza ya vuguvugu la mabadiliko, pamoja daima katika mkoa wa Pwani, mjini Kibaha kwa kuwahakikishia Watanzania kuwa wao sio Chama cha kidini na ni Chama cha kila Mtanzania mpenda mabadiliko chanya ya nchi.

Makamu wa Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, BW.ISSA MOHAMED amesema suala la udini ni agenda ya Chama tawala kutokana na kutumia kauli mbiu hiyo kujaribu kudhoofisha upinzani kama ilivyokuwa kwa chama cha wananchi-CUF- kwa kukiita chama hicho kuwa ni cha kidini.

Kwa kutumia propaganda ya ukanda walifanikiwa kuiporomosha CUF kwa kipindi hicho kwa kudai kuwa chama hicho ni chama cha Wapemba na walipoona kuwa haitoshi wakaanzisha propaganda kuwa chama hicho ni chama cha kidini na kufanikiwa kuwaweka pembeni katika mchakato wa kisiasa kuinganisha na mwanzo wake.

BW.MOHAMED amewaambia wana Pwani wamekuwa ndio chanzo cha CCM kuendelea kuwa madarakani kwa kutotoa fursa kwa vyama vingine kuongoza katika kanda hiyo, baada ya kukubali kugawanywa kikanda, kidini na kikabila.


Aidha alitumia nafasi hiyo kuwakumbusha Waislamu kutokubaliana na propaganda zinazotolewa na chama tawala ambazo zimekuwa zikiwatumia waislamu na amewaambia ishu sio uislamu na ishu ni audilifu na wakati umefika kwa wao kuona mambo katika mtazamo tofauti na awali ili kwa pamoja tuikombea Tanzania.
Amewataka Watanzania waliohudhuria mkutano huo katika viwanja vya mpira Maili moja kuwa ni vyema kukumbuka maneno ya mwasisi wa Taifa hili, MWL.NYERERE ambaye alisema kuwa kiongozi yoyote atakayekuja akajinasibu kwa ajili ya kabila lake au rangi yake au dini yake basi kiongozi huyo muogopeni kama ukoma.

Akiongea katika mkutano huo wa 105 toka kuanzishwa kwa vuguvugu la mabadiliko, pamoja daima, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, BW. FREEMAN MBOWE amesema kuwa wamezunguka maeneo mbalimbali ya Tanzania kasoro mikoa ya Lindi na Mtwara.

Bw.MBOWE ameeleza wameshindwa kufika huko kutokana na wananchi wa huko kuishi chini ya hali ya hatari kiasi cha kutoruhusiwa kwa mikutano ya kisiasa kufanyiika katika mikoa hiyo kutokana na wao kuthubutu kudai haki ya kufaidika na gesi iliyogunduliwa katika Mkoa wa Mtwara.

Operesheni hiyo imechukua takriban wiki mbili kwa lengo la kwenda kuwazindua Watanzania kuwa waache kulala usingizi kwani nchi yao inaliwa.

END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA