YPC YAPONGEZWA NA MKUU WA WILAYA-BIBI KIHEMBA
Ben Komba/Pwani-Tanzania/01-02-2014/12:39
Mkuu wa wilaya ya Kibaha BIBI.HALIMA KIHEMBA
ameyapongeza mashirika yasiyo ya kiserikali kwa kufanya kazi zao za kusaidia
serikali kutekeleza majukumu yake ya kila siku.
BIBI KIHEMBA akifunga kikao kati ya wakuu wa idara na
wakurugenzi wa halmashauri zote mbili za halmashauri ya mji na wilaya ya Kibaha
na Taasisi isiyo ya kiserikali ya YOUTH PARTNERSHIP COUNTRYWIDE, amesema kuwa
kwa sasa shughuli za mashirika yasiyo ya
kiserikali zimeanza kuzaa matunda.
Akizungumzia masuala mbalimbali ambayo yaliibuka
kufuatia mrejesho wa shughuli zilizotekelezwa na shirika lisilo la kiserikali
la YPC, Kuhusiana na migogoro ya wakulima na wafugaji, BIBI.KIHEMBA amefafanua kwa
kutoa mfano wa kijiji cha Gumba ambacho kina mgogoro mkubwa wa ardhi lakini
watendaji wa kijiji na kata wanangojea Mkuu wa wilaya atoe tamko.
Mkuu huyo wa wilaya BIBI.KIHEMBA ameongeza sheria kuhusu matumizi bora ya ardhi yapo
wazi na sheria zipo wazi lakini watendaji kwa sababu zisizo bayana wanashindwa
kutumia sheria zilizopo na kuzua sintofahamu katika jamii.
Naye Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la
YPC, BW.ISRAEL ILUNDE amesema katika mkutano huo wa mashauriano kuhusu
maendeleo na uwajibikaji kwa halmashauri mbili za wilaya ya Kibaha una lengo
kuwajengea uwezo vijana uwezo kupitia mradi SaVUKI ambao unaamanisha SAUTI YA
VIJANA KWENYE UWAJIBIKAJI WA KIJAMII kuchangia maendeleo ya nchi yao.
BW. ILUNDE ameongeza na katika utekelezaji wa mradi
huo ambao ulifanyika katika kipindi cha mwaka 2012 mpaka 2013, vijana na
makundi maalum ambayo yanaachwa nyuma na michakato mbalimbali ya kitaifa ili
waweze kujitambua na kufanya maamuzi sahihi tunapoelekea mwaka 2015.
Mkurugenzi huyo wa YPC ameongeza kuwa Katika
utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku wamekuwa wanashirikiana kwa karibu
naACTION AID TANZANIA
chini ya mpango wa uwajibikaji kwa umma-PUBLIC ACCOUNTABILITY PROJECT.
END.
Comments
Post a Comment