CCM KIBAHA MJINI YAONYA WAUZA MANENO
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/17 February 2014/
Wanachama wa
chama cha mapinduzi mjini Kibaha wametakiwa kutokuwa madalali wa kisiasa na
kuzua makundi ambayo yanhatarisha uhai wa chama katika kipindi hiki cha
kuelekea uchaguzi wa mitaa na baadaye wa uchaguzi mkuu mwaka 2015.
Mwenyekiti
wa CCM Kibaha mjini, BW.MAULID BUNDALA ameyasema hayo wakati akifungu kikao cha
baraza la wazazi Kibaha mjini, ambapo amesema kumekuwa kwa baadhi ya wana CCM
kupita huko na huko kutafuta watu wenye fedha na kuwashawishi kugombea nafasi
mbalimbali za uongozi.
Mwenyekiti
huyo wa CCM amebainisha kuwa cha kushangaza zaidi watu wanaowafuata wengi wao wanakuwa hawana
uzoefu katika siasa, na huku wakiwaacha makada wazoefu katika kuwapendekeza
katika kugombea nafasi mbalimbali kwa kuwa tu hawana fedha.
Aidha
ameongeza CCM imefikia mahali ina madalali wa kisiasa wanaoishi kwa kutegemea
kufanya utapeli wa kisiasa, kwa kutumia nafasi yao kama wanachama wa CCM kuuza
maneno kwa lengo la kujipatia mkate wao wa kila siku ilihali chama kinamong’onyoka.
Akifunga
kikao hicho cha Baraza la Wazazi, Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini, BW.SLYVESTER KOKA
amewasisitizia wajumbe wa Baraza la wazazi wa mjini Kibaha, kutotoa nafasi kwa
kamati ya wazee katika kusaidia kutuliza baadhi ya sintofahamu zinazojitokeza
katika Chama na Jumuiya zake.
BW.KOKA amewataka wana CCM kukaa vikao vya kikatiba
ili waweze kuimarisha Jumuiya hiyo ya chama katika kutekeleza ilani ya chama na
hapo ndipo watakapoweza kufanya vizuri katika chaguzi zijazo.
END.
Comments
Post a Comment