WANANCHI WAJITOLEA KUJENGA DARAJA KIBAHA.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/09:54/22/2/2014
Serikali ya
Mtaa wa Muheza katika halmashauri ya mji wa Kibaha kwa kushirikiana na wananchi
imeamua kujenga daraja kwa njia ya kujitolea ili kupunguza kero wanazopata
kipindi cha msimu wa mvua.
Mwenyekiti
wa serikali ya mtaa wa Muheza BW. MOHAMED LINGOWICHE amesema wameamua kuchukua
uamuzi kutokana na kero zinazowakabili kipindi cha mvua na kusababisha maisha
ya wananchi kuwa hatarini.
BW.LINGOWICHE
ameongeza kuwa kinachosaidia katika ujenzi huo wa makaravati ni kutokana na
wananchi wake kuwa wenye kuzingatia mambo na kumuelewa pale alipoitisha kikao cha
wananchi kuwaelezea kusudio la wananchi kujitolea kujenga makaravati hayo.
Amefafanua
kuwa Mbunge wa Jimbo la Kibaha, BW.SYLVESTER KOKA ametoa shilingi laki sita na
wananchi wakichangia shilingi laki 2, na kuwezesha kuchongwa kwa barabara hiyo
inayounganisha mtaa huo.
\Naye
Mwenyekiti wa Kamati ya Barabara Mtaa wa Muheza, BW. ASHRAF MMARI amesema mpaka
sasa ujenzi wa Makaravati umegharimu shilingi milioni 3.5,ili kuweza
kukamilisha ujenzi huo ambao jumla ya makaravati 9 yenye kipenyo cha mm 90, na
hivyo kuwezesha wananchi kupita kwa muda wote.
BW.MMARI
amefafanua kuwa wamekuwa wakipata michango mbalimbali ya fedha na vitendea
kazi, wakati mafundi wanaojenga makaravati hayo ni mafundi ambao wanaishi nao
mtaani na hivyo kurahisisha kwa kiasi kikubwa kazi hiyo ya kujitolea.
END.
Comments
Post a Comment