Posts

Showing posts from October, 2015

VIDEO=BBC NA MCT WAWANOA WANAHABARI UCHAGUZI MKUU

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/10/15/2015 6:56:17 AM Waandishi wa Habari  nchini wametakiwa kuhoji baadhi ya Habari mbalimbali zinazotolewa na baadhi ya vyombo vya Habari katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi ambazo zinaweza kusababisha uvinjifu wa amani. Mwezeshaji katika mafunzo ya waandishi wa Habari ambayo yameandaliwa na BBC MEDIA ACTION kuhusiana na uandishi wa Habari wenye kufuata maadili katika  kuripoti Habari za uchaguzi ambayo yamefanyika mjini Dar es Saalam, BW.ATTILIO TAGALILE amesema kuwa  vyombo vya Habari vimekuwa vikiripoti kuhusiana na mambo ambayo yanaweza kusababisha vurugu. BW.TAGALILE ameongeza kuwa kauli kama Goli la mkono au nitachukua nchi mapema asubuhi kwa kauli kama hizo ambazo jamii inazipata kupitia vyombo vya Habari na kutozifanyia kazi ikiwa pamoja na Tume ya uchaguzi na waandishi wa Habari wenyewe kwani  walikuwa na wajibu wa kufuatilia ili kupata ufafanuzi jinsi gani wanaweza kutekeleza goli la mkono na vipi itawezekana ushindi mapema asubuh

KILIO CHA MAJI MAJI MAJI KILA SEHEMU

Ben Komba/Pwani-Tanzania/10/15/2015 11:44:15 AM Wananchi katika Kata ya Vigwaza kijiji cha Kitonga wilayani Bagamoyo wamepaza sauti kutokana na kukabiliwa na ukosefu wa maji kwa kipindi kirefu toka Halmashauri ilpodai kuboresha miundo mbinu ya maji ili kuwasaidia wananchi kupata maji safi na ya uhakika. Mwandishi wa Habari hizi akiongea na wakazi wa eneo ambao kila mmoja ameeleza kushamiri kwa kero ya kijijini hapo toka halamshauri ya wilaya Bagamoyo ambayo ilipeleka mradi wa maboresho ya miundombinu ya maji lakini ikawa tofauti. Mzee maarufu kijijini Kitonga, KOMREDI NDALO amebainisha kuwa halmashauri ilitoa kiasi cha shilingi milioni 261 kwa ajili ya kusambaza maji katika kijiji hicho kilicho hatua chache kutoka mtambo wa maji wa Ruvu juu, lakini kilichofanyika imekuwa kinyume ambapo ule mtandao wa awali wa maji ambao ulikuwa na bomba kubwa na kuasidia wananchiu ulivurugwa na kusababisha kukoseka kwa maji kabisa. KOMREDI NDALO amebainisha kuwa mkandarasi huyo ambaye

WAANDISHA WANOLEWA TAYARI KWA UCHAGUZI

Ben Komba/Pwani-Tanzania/10/15/2015 6:56:17 AM Waandishi wa Habari  nchini wametakiwa kuhoji baadhi ya Habari mbalimbali zinazotolewa na baadhi ya vyombo vya Habari katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi ambazo zinaweza kusababisha uvinjifu wa amani. Mwezeshaji katika mafunzo ya waandishi wa Habari ambayo yameandaliwa na BBC MEDIA ACTION kuhusiana na uandishi wa Habari wenye kufuata maadili katika  kuripoti Habari za uchaguzi ambayo yamefanyika mjini Dar es Saalam, BW.ATTILIO TAGALILE amesema kuwa  vyombo vya Habari vimekuwa vikiripoti kuhusiana na mambo ambayo yanaweza kusababisha vurugu. BW.TAGALILE ameongeza kuwa kauli kama Goli la mkono au nitachukua nchi mapema asubuhi kwa kauli kama hizo ambazo jamii inazipata kupitia vyombo vya Habari na kutozifanyia kazi ikiwa pamoja na Tume ya uchaguzi na waandishi wa Habari wenyewe kwani  walikuwa na wajibu wa kufuatilia ili kupata ufafanuzi jinsi gani wanaweza kutekeleza goli la mkono na vipi itawezekana ushindi mapema asubuhi.

WAANDISHI WANOLEWA KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/10/15/2015 6:56:17 AM Waandishi wa Habari  nchini wametakiwa kuhoji baadhi ya Habari mbalimbali zinazotolewa na baadhi ya vyombo vya Habari katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi ambazo zinaweza kusababisha uvinjifu wa amani. Mwezeshaji katika mafunzo ya waandishi wa Habari ambayo yameandaliwa na BBC MEDIA ACTION kuhusiana na uandishi wa Habari wenye kufuata maadili katika  kuripoti Habari za uchaguzi ambayo yamefanyika mjini Dar es Saalam, BW.ATTILIO TAGALILE amesema kuwa  vyombo vya Habari vimekuwa vikiripoti kuhusiana na mambo ambayo yanaweza kusababisha vurugu. BW.TAGALILE ameongeza kuwa kauli kama Goli la mkono au nitachukua nchi mapema asubuhi kwa kauli kama hizo ambazo jamii inazipata kupitia vyombo vya Habari na kutozifanyia kazi ikiwa pamoja na Tume ya uchaguzi na waandishi wa Habari wenyewe kwani  walikuwa na wajibu wa kufuatilia ili kupata ufafanuzi jinsi gani wanaweza kutekeleza goli la mkono na vipi itawezekana ushindi mapema asubuhi.

KIPINDI MAALUM-MAJI TATIZO LA KITAIFA ANGALIA HALI ILIVYO.

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/10/12/2015 11:52:08 AM Suala la ukosefu wa maji katika maeneo mbalimbali nchini linaelekea katika kusababisha uvunjifu wa amani kama hatua za makusudi hazitachukuliwa kukabiliana na hali hiyo. Mwandishi wa Habari hizi ameshuhudia dhahama kubwa kati ya wananhi ambao kwa miaka mingi wameishi kama majirani wamejikuta wanalazimika kukunjiana ngumi na jirani mwenzie kisa maji, ambayo yamekuwa lulu maeneo mengine ya mkoa wa Pwani. Sintofahamu hiyo imejitokeza katika kijiji cha Kiluvya madukani A, katika wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani, Ambapo kwa mujibu wa msimamizi wa kiosk cha kuuza maji BW.RAYMOND KOBELO ambacho kilibuniwa na Waziri Mkuu Mstaafu, MH.FREDIRICK SUMAYE ili kuwasaidia wakazi wa eneo hilo. BW.KOBELO amejitetea kuwa Bomba hilo limewekwa kwa hisani ya Waziri mkuu mstaafu na hicho ni moja ya vituo vinne ambavyo vilifunguliwa katika wakati huo, hatua ya wananchi kutaka kuchukua mita ya maji ya kituo hicho na kupeleka kituo kingine yeye

MAJI YASABABISHA UVINJIFU WA AMANI

Ben Komba/Pwani-Tanzania/10/12/2015 11:52:08 AM Suala la ukosefu wa maji katika maeneo mbalimbali nchini linaelekea katika kusababisha uvunjifu wa amani kama hatua za makusudi hazitachukuliwa kukabiliana na hali hiyo. Mwandishi wa Habari hizi ameshuhudia dhahama kubwa kati ya wananhi ambao kwa miaka mingi wameishi kama majirani wamejikuta wanalazimika kukunjiana ngumi na jirani mwenzie kisa maji, ambayo yamekuwa lulu maeneo mengine ya mkoa wa Pwani. Sintofahamu hiyo imejitokeza katika kijiji cha Kiluvya madukani A, katika wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani, Ambapo kwa mujibu wa msimamizi wa kiosk cha kuuza maji BW.RAYMOND KOBELO ambacho kilibuniwa na Waziri Mkuu Mstaafu, MH.FREDIRICK SUMAYE ili kuwasaidia wakazi wa eneo hilo. BW.KOBELO amejitetea kuwa Bomba hilo limewekwa kwa hisani ya Waziri mkuu mstaafu na hicho ni moja ya vituo vinne ambavyo vilifunguliwa katika wakati huo, hatua ya wananchi kutaka kuchukua mita ya maji ya kituo hicho na kupeleka kituo kingine yeye h

VIDEO-ACT WAZALENDO WATAKA NEC IWE MACHO NA VITENDO VYA VURUGU KIPINDI CHA KAMPENI.

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/10/5/2015 11:23:20 AM Chama cha ACT-WAZALENDO katika mkoa wa Pwani wamekemea tabia ya baadhi ya vyama kufanya vurugu katika mikutano ya kampeni ya chama chao kama ilivyojitokeza mjini Kibaha. Akizungumza na mwandishi wa Habari hizi, Katibu wa ACT-WAZALENDO mkoa wa Pwani, NDUGU MRISHO HALFAN amesema kuwa kitendo cha wananchama wa Chama cha CHADEMA kuvamia kikao cha kampeni cha mgombea ubunge wao na kufanya fujo. NDUGU HALFAN ameongeza anashangwaza na tabia za baadhi ya wanachama wa CHADEMA kujitokeza katika mikutano yao kwa lengo la kufanya vurugu, kitu ambacho amebainisha hawataweza kuendelea kuvumilia hali hiyo. Katibu huyo wa ACT-WAZALENDO ,NDUGU HALFAN ameongeza kwamba ni wajibu wa Jeshi la Polisi kuhakikisha kuwa linadhibiti vitendo hivyo vinavyoashiria uvunjifu wa amani. Aidha ametumia nafasi hiyo kutoa pole kwa wanachama wa chama cha DEMOCRATIC PARTY, kufuatia kupatwa na msiba wa Mwenyekiti wao, Mchungaji CHRISTOPHER MTIKILA amba

MCHUNGAJI MTIKILA AFARIKI AJALINI.

SUNDAY, OCTOBER 4, 2015 MCH MTIKILA AFARIKI AJALINI Na John Gagarini, Chalinze   MWANASIASA Mkongwe hapa nchini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama ChaDemocratic Party (DP) Mchungaji Christopher Mtikila (62) amefariki dunia na watu wengine watatu kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka.   Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi mkoani Pwani Jafary Mohamed alisema kuwa tukio hilo lilitokea huko Msolwa Barabara Kuu ya Dar es Salaam Morogoro wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.   Kamanda Mohamed alisema kuwa ajali hiyo ilitokea saa 11:45 Alfajiri wakitokea mkoani Njombe wakiwa na gari aina ya Toyota Corola lenye namba za usajili T189 AGM lililokuwa likiendeshwa na dereva aitwaye George Steven (31) maarufu Ponera mkazi wa Mbezi Jijini Dar es Salaam.   "Gari hilo likiwa na abiria watatuakiwemo marehemu mkazi wa Mikocheni B, lilikuwa kwenye mwendo wa kasi liliacha njia na kuserereka pembeni mwa barabara kasha kupinduka ambapo marehemu ali

VIDEO-MAMA REGINA LOWASSA AKUMBANA NA VURUGU ZIARA YAKE KIBAHA VIJIJINI.

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/10/3/2015 9:07:43 AM Ujio wa Mama REGINA LOWASSA katika Jimbo la uchaguzi Kibaha vijijini umekumbwa na vurugu ambazo kama isingekuwa busara ya wanachama wa CHADEMA basi pangezuka vita. Kadhia hiyo imeanza mara baada ya Mama Lowassa kuwasili ofisi ya Jimbo la Chama hicho Kibaha vijijini kwa ajili ya kutia saini kitabu cha wageni ili baadaye aende kukagua sehemu alizopangiwa. Lakini hali haikuwa rahisi kutoka ofisini hapo baada ya kundi la wanaCCM kutokea na kuziba barabra ambayo angekuwa aitumie kuondoka ofisini hapo na hivyo kusababisha kusukumana kwa wananchama wa vyama hivyo viwili. Huku CCM wakiongozwa na mchumi wa Jumuiya ya wazazi mkoa wa Pwani, BW.HAJI ABUU JUMA ambapo walisababisha mtafaruku tosha ambao kama isingekuwa busara ya CHADEMA basi kampeni zingeingia doa. END. 

VIDEO-ACT WAZALENDO YA PILI KWA KUSIMAMISHA WAGOMBEA WENGI NYUMA YA CCM

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/10/2/2015 2:13:19 PM Vijana wametakiwa kutojiweka nyuma katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi kwa kujitokeza na kufanya maamuzi ambayo yataletea Taifa tija kutokana na wao kuwa na mchango mkubwa katika ujenzi wa Taifa. Hayo yamezungumzwa na mgombea ubunge kupitia tiketi ya ACT-WAZALENDO katika Jimbo la uchaguzi Bukoba vijijini, BW. ABDUL RUSHAKA akiwa mmoja ya vijana ambao kwa kutokana na ujasiri alionao ameamua kujitosa kupambana kumng’oa mbunge ambaye amemaliza muda wake. BW.RUSHAKA amesema ingekuwa vyema iwapo wananchi wakiamua kufanya mabadiliko ili kuliletea Taifa maendeleo ambayo yamekuwa yanasubiriwa kwa takribani miaka 50 sasa ambapo amewasisitiza vijana kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo la kihistoria. BW.RUSHAKA amewasihi wapinzani wote ambao wapo ndani ya UKAWA na nje ya UKAWA kuunganisha nguvu ili kuwang’oa chama tawala ambao mpaka sasa wamejenga tabia ya kuwa wao hawawezi kushi mpaka wawe watawala na kuwataka wapinzani ku

ADHA YA MAJI BAGAMOYO.

Image
ADHA YA MAJI KIJIJI CHA GONGO KATA YA MKANGE JIMBO LA CHALINZE WILAYA YA BAGAMOYO PWANI Na John Gagarini, Mkange WANANCHI wa Kijiji cha Gongo kata ya Mkange wilayani Bagamoyo wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji ambapo huweka foleni ya kuchota maji kwenye kisima kilichopo kijijini hapo baada ya wiki mbili. Kutokana na usosefu huo wa maji wananchi hao wamekuwa wakinunua maji ya bomba ndoo ya lita 20 kati ya shilingi 1,000 na shilingi 1,500 maji ambayo huuzwa kwenye magari au pikipiki hivyo kuwafanya wajikute hawapati maendeleo kutokana na gharama kubwa kuzitumia kununulia maji. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mkutano wa kampeni wa mgombea Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhiwani Kikwete, kwenye kata ya Mkange mwananchi wa Kijiji hicho Hungilo Nyoka alisema kuwa maji yamewafanya washindwe kupata maendeleo. Nyoka alisema kila kaya inatakiwa ichote madumu manne ili angalau kila mmoja apate baada ya hapo maji hukatika ambapo in

ACT WAZALENDO NAO WANATISHA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/10/2/2015 2:13:19 PM Vijana wametakiwa kutojiweka nyuma katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi kwa kujitokeza na kufanya maamuzi ambayo yataletea Taifa tija kutokana na wao kuwa na mchango mkubwa katika ujenzi wa Taifa. Hayo yamezungumzwa na mgombea ubunge kupitia tiketi ya ACT-WAZALENDO katika Jimbo la uchaguzi Bukoba vijijini, BW. ABDUL RUSHAKA akiwa mmoja ya vijana ambao kwa kutokana na ujasiri alionao ameamua kujitosa kupambana kumng’oa mbunge ambaye amemaliza muda wake. BW.RUSHAKA amesema ingekuwa vyema iwapo wananchi wakiamua kufanya mabadiliko ili kuliletea Taifa maendeleo ambayo yamekuwa yanasubiriwa kwa takribani miaka 50 sasa ambapo amewasisitiza vijana kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo la kihistoria. BW.RUSHAKA amewasihi wapinzani wote ambao wapo ndani ya UKAWA na nje ya UKAWA kuunganisha nguvu ili kuwang’oa chama tawala ambao mpaka sasa wamejenga tabia ya kuwa wao hawawezi kushi mpaka wawe watawala na kuwataka wapinzani kutopo