VIDEO=BBC NA MCT WAWANOA WANAHABARI UCHAGUZI MKUU
Ben Komba/Pwani-Tanzania/10/15/2015 6:56:17 AM
Waandishi wa Habari
nchini wametakiwa kuhoji baadhi ya Habari mbalimbali zinazotolewa na
baadhi ya vyombo vya Habari katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi ambazo
zinaweza kusababisha uvinjifu wa amani.
Mwezeshaji katika
mafunzo ya waandishi wa Habari ambayo yameandaliwa na BBC MEDIA ACTION
kuhusiana na uandishi wa Habari wenye kufuata maadili katika kuripoti
Habari za uchaguzi ambayo yamefanyika mjini Dar es Saalam, BW.ATTILIO TAGALILE
amesema kuwa vyombo vya Habari vimekuwa vikiripoti kuhusiana na mambo
ambayo yanaweza kusababisha vurugu.
BW.TAGALILE ameongeza
kuwa kauli kama Goli la mkono au nitachukua nchi mapema asubuhi kwa kauli kama
hizo ambazo jamii inazipata kupitia vyombo vya Habari na kutozifanyia kazi
ikiwa pamoja na Tume ya uchaguzi na waandishi wa Habari wenyewe kwani
walikuwa na wajibu wa kufuatilia ili kupata ufafanuzi jinsi gani wanaweza
kutekeleza goli la mkono na vipi itawezekana ushindi mapema asubuhi.
Hivyo amewaasa
waandishi wa Habari kueppuyka kuandika Habari kama hizo na hasa ikizingatiwa
Jumuiya ya kimataifa inafuatilia kwa karibu mchakato wa uchaguzi mkuu
unavyoendelea, na iwapo ikitokea kukatokea vurugu waandishi, chanzo cha maneno
hayo basi mahakama ya uhalifu ya kimataifa itawahusu, na kuwasisitizia kuwa
makini na kuepuka matatizo kama yaliyomkuta mwandishi wa Kenya, NDG.ARAP SANG.
Naye mshiriki wa
mafunzo hayo, BI.SALMA MKALIBALA amewapongeza BBC MEDIA ACTION kwa kuweza kutoa
mafunzo hayo ambayo kwa njia moja au nyingine yamemfumbua macho juu umakini
kipindi cha kuripoti Habari za uchaguzi ili kuepuka kukiuka maadili ya
taaluma.
Mafunzo hayo ambayo
yamejumuisha waandishi wa Habari kutoka mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani na
Tanga, na yaliandaliwa na BBC MEDIA ACTION na Baraza la Habari Tanzania.
END.
Comments
Post a Comment