MAJI YASABABISHA UVINJIFU WA AMANI
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/10/12/2015 11:52:08 AM
Suala la
ukosefu wa maji katika maeneo mbalimbali nchini linaelekea katika kusababisha
uvunjifu wa amani kama hatua za makusudi hazitachukuliwa kukabiliana na hali
hiyo.
Mwandishi wa
Habari hizi ameshuhudia dhahama kubwa kati ya wananhi ambao kwa miaka mingi
wameishi kama majirani wamejikuta wanalazimika kukunjiana ngumi na jirani
mwenzie kisa maji, ambayo yamekuwa lulu maeneo mengine ya mkoa wa Pwani.
Sintofahamu hiyo
imejitokeza katika kijiji cha Kiluvya madukani A, katika wilaya ya Kisarawe
mkoa wa Pwani, Ambapo kwa mujibu wa msimamizi wa kiosk cha kuuza maji BW.RAYMOND
KOBELO ambacho kilibuniwa na Waziri Mkuu Mstaafu, MH.FREDIRICK SUMAYE ili
kuwasaidia wakazi wa eneo hilo.
BW.KOBELO
amejitetea kuwa Bomba hilo limewekwa kwa hisani ya Waziri mkuu mstaafu na hicho
ni moja ya vituo vinne ambavyo vilifunguliwa katika wakati huo, hatua ya
wananchi kutaka kuchukua mita ya maji ya kituo hicho na kupeleka kituo kingine
yeye hakubaliani nacho.
Bw. KOBELO ameita
Hatua ya wananchi kutaka kuchukua mita kutoka katika kituo hicho na kuipeleka
katika kituo kipya kilichoanzishwa na nguvu za wananchi ni sawa na wao kujichanganya toka mita hiyo
ipo kwa jina lake, hivyo amewataka wananchi kufuatilia mita DAWASCO.
Akiongea katika
tukio hilo mtumishi wa DAWASCO, Kisarawe BW.BWIRE MARWA amewataka wananchi hao
kupunguza jazba wakati yeye atakapoenda kumshauri meneja wa DAWASCO Kisarawe,
kuangalia uwezekano wa wananchi hao kupatiwa mita ya maji kama bodi ya maji ya
kitongoji hicho inavyotaka.
Katibu wa
Bodi ya maji kitongoji Kiluvya madukani A, BIBI .MARIETHA KAVISHE amesema kuwa
wao kama wahusika wa maji katika kitongoji chao, wamekuwa wakipokea malalamiko
mbalimbali kutoka kwa wananchi.
BIBI.KAVISHE
amefafanua kuwa wananchi wengi wamekuwa wakidai kuwa mara nyingine wamekuwa
wanatukanwa wanapokwenda kuchota maji katika kituo hicho ikiwqa pamoja na
sharti la kuchota maji mwisho saa 12 jioni.
BIBI.
KAVISHE ameongeza kitu ambacho wananchi kimewakasirisha ni unit za maji
kuongezeka tofauti na wanapoziacha siku ya mwisho na kugundua kuwa kuna ujanja Fulani
umefanyika na kujikuta wananchi wanaibiwa fedha zao bila kujijua, na kulazimika
kulipa bili mpaka shilingi 70,000/=
END.
Comments
Post a Comment