KILIO CHA MAJI MAJI MAJI KILA SEHEMU

Ben Komba/Pwani-Tanzania/10/15/2015 11:44:15 AM

Wananchi katika Kata ya Vigwaza kijiji cha Kitonga wilayani Bagamoyo wamepaza sauti kutokana na kukabiliwa na ukosefu wa maji kwa kipindi kirefu toka Halmashauri ilpodai kuboresha miundo mbinu ya maji ili kuwasaidia wananchi kupata maji safi na ya uhakika.

Mwandishi wa Habari hizi akiongea na wakazi wa eneo ambao kila mmoja ameeleza kushamiri kwa kero ya kijijini hapo toka halamshauri ya wilaya Bagamoyo ambayo ilipeleka mradi wa maboresho ya miundombinu ya maji lakini ikawa tofauti.

Mzee maarufu kijijini Kitonga, KOMREDI NDALO amebainisha kuwa halmashauri ilitoa kiasi cha shilingi milioni 261 kwa ajili ya kusambaza maji katika kijiji hicho kilicho hatua chache kutoka mtambo wa maji wa Ruvu juu, lakini kilichofanyika imekuwa kinyume ambapo ule mtandao wa awali wa maji ambao ulikuwa na bomba kubwa na kuasidia wananchiu ulivurugwa na kusababisha kukoseka kwa maji kabisa.

KOMREDI NDALO amebainisha kuwa mkandarasi huyo ambaye alikuwa anakwenda kwa jina SAJO,alichofanya ni kuweka mabomba madogo ambayo hayana uwezo wa kusambaza maji kutokana nguvu yaliyonayo na kusababisha kupasuka kwa mabomba na hivyo kuwalazimu wananchi kunywa maji ya tope.

Akizungumzia suala ukosefu wa maji, Mgombea wa ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya UKAWA, BW.MATHAYO TORENGEY amewaambia wananchi wa Kitonga kuwa suala la ukosefu wa maji atalipa kupaumbele mkubwa hasa kutokana na serikali ya CCM kushindwa kufanya hivyo.

BW. TORENGEY amewataka wananchi kumpa fursa ya kuwa Mbunge wao ili aweze kuwasaidia kutatua baadhi ya kero ambazo zinawakabili.

END.


Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA