KIPINDI MAALUM-MAJI TATIZO LA KITAIFA ANGALIA HALI ILIVYO.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/10/12/2015 11:52:08 AM
Suala la
ukosefu wa maji katika maeneo mbalimbali nchini linaelekea katika kusababisha
uvunjifu wa amani kama hatua za makusudi hazitachukuliwa kukabiliana na hali
hiyo.
Mwandishi wa
Habari hizi ameshuhudia dhahama kubwa kati ya wananhi ambao kwa miaka mingi
wameishi kama majirani wamejikuta wanalazimika kukunjiana ngumi na jirani
mwenzie kisa maji, ambayo yamekuwa lulu maeneo mengine ya mkoa wa Pwani.
Sintofahamu
hiyo imejitokeza katika kijiji cha Kiluvya madukani A, katika wilaya ya
Kisarawe mkoa wa Pwani, Ambapo kwa mujibu wa msimamizi wa kiosk cha kuuza maji
BW.RAYMOND KOBELO ambacho kilibuniwa na Waziri Mkuu Mstaafu, MH.FREDIRICK
SUMAYE ili kuwasaidia wakazi wa eneo hilo.
BW.KOBELO
amejitetea kuwa Bomba hilo limewekwa kwa hisani ya Waziri mkuu mstaafu na hicho
ni moja ya vituo vinne ambavyo vilifunguliwa katika wakati huo, hatua ya
wananchi kutaka kuchukua mita ya maji ya kituo hicho na kupeleka kituo kingine
yeye hakubaliani nacho.
Bw. KOBELO
ameita Hatua ya wananchi kutaka kuchukua mita kutoka katika kituo hicho na
kuipeleka katika kituo kipya kilichoanzishwa na nguvu za wananchi ni sawa na wao kujichanganya toka mita hiyo
ipo kwa jina lake, hivyo amewataka wananchi kufuatilia mita DAWASCO.
Akiongea
katika tukio hilo mtumishi wa DAWASCO, Kisarawe BW.BWIRE MARWA amewataka
wananchi hao kupunguza jazba wakati yeye atakapoenda kumshauri meneja wa
DAWASCO Kisarawe, kuangalia uwezekano wa wananchi hao kupatiwa mita ya maji
kama bodi ya maji ya kitongoji hicho inavyotaka.
Katibu wa
Bodi ya maji kitongoji Kiluvya madukani A, BIBI .MARIETHA KAVISHE amesema kuwa
wao kama wahusika wa maji katika kitongoji chao, wamekuwa wakipokea malalamiko
mbalimbali kutoka kwa wananchi.
BIBI.KAVISHE
amefafanua kuwa wananchi wengi wamekuwa wakidai kuwa mara nyingine wamekuwa
wanatukanwa wanapokwenda kuchota maji katika kituo hicho ikiwqa pamoja na
sharti la kuchota maji mwisho saa 12 jioni.
BIBI.
KAVISHE ameongeza kitu ambacho wananchi kimewakasirisha ni unit za maji
kuongezeka tofauti na wanapoziacha siku ya mwisho na kugundua kuwa kuna ujanja
Fulani umefanyika na kujikuta wananchi wanaibiwa fedha zao bila kujijua, na
kulazimika kulipa bili mpaka shilingi 70,000/=
END.
Comments
Post a Comment