VIDEO-ACT WAZALENDO YA PILI KWA KUSIMAMISHA WAGOMBEA WENGI NYUMA YA CCM
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/10/2/2015 2:13:19 PM
Vijana
wametakiwa kutojiweka nyuma katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi kwa
kujitokeza na kufanya maamuzi ambayo yataletea Taifa tija kutokana na wao kuwa
na mchango mkubwa katika ujenzi wa Taifa.
Hayo yamezungumzwa
na mgombea ubunge kupitia tiketi ya ACT-WAZALENDO katika Jimbo la uchaguzi
Bukoba vijijini, BW. ABDUL RUSHAKA akiwa mmoja ya vijana ambao kwa kutokana na
ujasiri alionao ameamua kujitosa kupambana kumng’oa mbunge ambaye amemaliza
muda wake.
BW.RUSHAKA
amesema ingekuwa vyema iwapo wananchi wakiamua kufanya mabadiliko ili kuliletea
Taifa maendeleo ambayo yamekuwa yanasubiriwa kwa takribani miaka 50 sasa ambapo
amewasisitiza vijana kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo la kihistoria.
BW.RUSHAKA
amewasihi wapinzani wote ambao wapo ndani ya UKAWA na nje ya UKAWA kuunganisha
nguvu ili kuwang’oa chama tawala ambao mpaka sasa wamejenga tabia ya kuwa wao
hawawezi kushi mpaka wawe watawala na kuwataka wapinzani kutopoteza muda
kugombana wenyewe kwa wenyewe badala ya kumlenga adui yao mkuu ambaye ni chama
tawala.
END
Comments
Post a Comment