Posts

Showing posts from April, 2012

BABA ATELEKEZA FAMILIA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/Wednesday, April 11, 2012/.06:48:08 PM Mama mmoja mkazi wa mjini Kibaha BI. DIGNA LAURENT MASHAKAhivi karibuni amekumbwa na kisanga cha kutelekezewa watoto na mali za familia kuuzwa na mume wake wa ndoa, kwa sababu ya ndoa yao kuingiliwa na Mama mmoja mjane mkristo wa TAG anayejulikana kwa jina la Mama BETTY ambaye awali alikuwa anadai ana undugu na Mume wa mlalamikaji lakini kumbe ni kinyume chake. BI. DIGNA MASHAKA amebainisha mgogoro ulianza kwa yeye kuitwa mchawi na mume wake, na katika madai yake hayo siku moja mumewe BW. LAURENT MASHAKA (Michuzi) alirudi nyumbani na kumwita aende chumbani na mara alivyoingia akaanza kumkaba kiasi cha majirani kujitokeza na kuja kumuamulia, huku akidai ameweka uchawi kwenye viatu vyake na hivyo kumsababishia kupata fangasi. Na kutokana na tukio hilo BI.DIGNA MASHAKA aliamua kufungua kesi ya dhidi ya mume wake akilalamikia kitendo kilichofanywa naye, na lengo sio kuachana na mumewe, lakini kesi hiyo iliendeshwa kw

BAJETI YA HALMASHAURI WILAYA KIBAHA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/Tuesday, 10 April, 2012/6:46:32 PM Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2012/2013 halmashauri ya wilaya ya Kibaha imepanga kutumia jumla ya shilingi bilioni 14.8 ambapo kati ya fedha hizo ni shilingi bilioni 12 ndizo zitakazotoka serikali kuu. Hayo yamesemekana katika kikao maalum cha bajeti cha baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Kibaha, wakati Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, BW. CHRISTOPHER MDUMA alipokuwa anawasilisha makisio na makadirio ya mapato na matumizi katika kipindi cha mwaka 2012/2013. BW.MDUMA amesema kati ya fedha hizo ambazo zimeanishwa katika bajeti hiyo, shilingi bilioni 2.5 ikiwa ni makusanyo ya ndani na ikiwa pamoja na michango ya jamii na nguvukazi yao ikiwa zaidi ya shilingi bilioni 10. BW. MDUMA akizungumzia upande wa mishahara amefafanua zaidi ya shilingi bilioni 8 zimetengwa upande huo, na matumizi ya kawaida yanakadiriwa kufikia shilingi bilioni 2.8 na miradi ya maendeleo ikiwa imetengewa shilingi bilioni 3.6. Awal

MTENGEZA GOBOLE MBARONI

Ben Komba/Pwani-Tanzania/Thursday, 05 April, 2012/05:03:05 PM Kamanda wa Polisi mkoani Pwani ERNEST MANGU ametoa wito kwa wataalam ambao wana uwezo wa kutengeneza bunduki kujitokeza hadharani ili kufuata taratibu za kisheria ili kuepuka mkono wa sheria badala ya kufanya kazi zao kwa kificho hali ambayo inaongeza wimbi la wizi wa kutumia silaha. Kamanda MANGU amesema kwa mtu yoyote ambaye anajua ana uwezo wa kutengeneza bunduki kuwasiliana na ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri aliyopo ili kupatiwa kibali ambacho kitamtambulisha kisheria kuhusika kwake kwa kazi hiyo, na vibali hivyo watawjibnika kuvilipia kila mwaka kama sheria inavyoelekeza na hivyo kuepusha uwezekano wa wataalamu hao kutmika sivyo na wahalifu. KAMANDA MANGU ameyazungumza hayo kufuatia kugundulika kwa kiwanda mwitu cha kutengeneza silaha kilichokuwa kikimilikiwa na BW. PETRO MAZIKU, katika eneo Mamdikongo kitongoji cha TABORA wilayani Mkuranga, ambapo mkazi huyto alikutwa na bunduki aina ya magobole yanayokaribia

RIPOTI YA MTOTO ALIBAKWA YATHIBITISHA NDIVYO.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/4/1/2012 6:44:26 PM Taarifa ya daktari kuhusiana na tukio la kubakwa kwa mtoto wa mwenye umri wa miaka 3 na miezi minane ambalo limetokea March 27 mwaka huu imeshatolewa na kuthibitisha kuwa ni kweli mtoto huyto alifanyiwa kitendo hicho cha kikatili na kijana huyo ambaye anadaiwa kuwa na miaka zaidi ya 20. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mama wa mtoto huyo, BI. ASHURA WAZIR amesema majibu hayo ambayo yanafuatiwa uchunguzi uliofanyika katika Hospitali teule ya mkoa ya Tumbi. Na kwa mujibu wa vyeti hivyo ambavyo mwandishi wa habari hizi ameviona vinaonyesha kuwa mtoto huyo amekutwa na michubuko meneo ya siri, damu na mbegu mbichi za kiume zinaaokadiriwa gramu 1. Cheti hicho namba:MFM 40 na namba ya uandikishaji 004 kilichotolewa hospitali ya Tumbi, kimeonyesha pia dawa alizopewa mtoto baada ya msukosuko huo ni PANADOL, Akashauriwa kuogea DETTOL, Erythromycin na kutakiwa kuhudhuria kituo cha kupima UKIMWI na kumuona mganga bingwa wa magonjwa ya kina