MTENGEZA GOBOLE MBARONI

Ben Komba/Pwani-Tanzania/Thursday, 05 April, 2012/05:03:05 PM Kamanda wa Polisi mkoani Pwani ERNEST MANGU ametoa wito kwa wataalam ambao wana uwezo wa kutengeneza bunduki kujitokeza hadharani ili kufuata taratibu za kisheria ili kuepuka mkono wa sheria badala ya kufanya kazi zao kwa kificho hali ambayo inaongeza wimbi la wizi wa kutumia silaha. Kamanda MANGU amesema kwa mtu yoyote ambaye anajua ana uwezo wa kutengeneza bunduki kuwasiliana na ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri aliyopo ili kupatiwa kibali ambacho kitamtambulisha kisheria kuhusika kwake kwa kazi hiyo, na vibali hivyo watawjibnika kuvilipia kila mwaka kama sheria inavyoelekeza na hivyo kuepusha uwezekano wa wataalamu hao kutmika sivyo na wahalifu. KAMANDA MANGU ameyazungumza hayo kufuatia kugundulika kwa kiwanda mwitu cha kutengeneza silaha kilichokuwa kikimilikiwa na BW. PETRO MAZIKU, katika eneo Mamdikongo kitongoji cha TABORA wilayani Mkuranga, ambapo mkazi huyto alikutwa na bunduki aina ya magobole yanayokaribia ubora wa bunduki ya SHOTGUN, kutokana na bunduki anazotengeneza yeye kutumia risasi za bunduki hiyo. Mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote pale uchunguzi utakapokamilika. END. STORY 2 MAZINGIRA Chama cha waandishi wa habari za mazingira na watu wenye ulemavu Pwani (PEDWA) kimewataka watanzania kutumia nishati ya gesi kama ni nishati mbadala ya mkaa, kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya bidhaa hiyo inayotokana na miti. Akizungumza mara baada ya kupatiwa semina kuhusiana na matumizi ya gesi ya ORYX kwa ajili ya shughuli mbalimbali na unafuu wake kulinganisha na mkaa, Makamu mwenyekiti wa PEDWA amesema hayo wakati wa mahojiano na mwandishi wa RFA, kuwa wao kama waandishi wameshawishika kwa kiasi kikubwa kufanyia kazi masuala ya mazingira kutokana na kitisho kinachosababishwa na uchomaji mkaa. BW. MSAFIR amebainisha kuwa kumekuwepo na ufahamu mdogo juu ya matumizi sahihi ya gesi kwa watanzania walio wengi, na wengi wao wakichukulia matumizi ya gesi kama ni anasa na aghali, hali ambayo amesema siyo kweli kutokana utafiti ambao umefanywa na wadau mbalimbali, hivyo amewahimiza wanahabari kutumia kalamu zao vizuri kutafuta njia ambazo zitampunguzia mtanzania wa kawaida makali ya uchumi yanayowakabili watanzania walio wengi. BW. MSAFIR SANJITO amesema iwapo mtungi wa gesi wa kilo 6 unaweza kutumika kwa siku 28 ambapo gharama yake ni shilingi elfu 24 tu, ambapo kama ukitumia mkaa inakupasa kutumia gunia 4 ambazo kwa sasa moja linauzwa shilingi elfu 15 mpaka elfu ishirini, kwa magunia manne ya mkaa yanagharimu zaidi ya shilingi elfu 60 za kitanzania kwa mwezi. Naye mwakilishi wa ofisa masoko wa Kampuni ya gesi ya ORYX, BI. MONICA JOHN amesema amefurahishwa na hatua ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Pwani kuunda chama hicho, na wao kama ORYX watahakikisha wanabadilishana uzoefu ili kuipatia elimu jamii kuhusiana na matumizi ya gesi kwa ajili ya kupikia na kuwashia taa ili kupunguza utegemezi wa mkaa. BI. MONICA JOHN amebainisha kuwa mkoa wa Dar es saalam kwa siku unatumia zaidi ya magunia 40,000 ya mkaa ambao mwingi unatoka katika mkoa wa Pwani, sehemu ambayo matumizi ya gesi yapo chini kabisa na hivyo kusababisha kuongezeka kwa uharibifu wa mazingira kutokana na ukataji ovyo wa miti. Amebainisha kuwa ili upate gunia moja la mkaa, mkata mkaa hana budi kuangusha miti 3, kutokana na Kampuni ya gesi ya ORYX kuliona hilo imeamua kujikita katika kuhamasisha matimizi ya gesi kwa jamii hususan inayoishi pembezoni kwa kuhakikisha nao pia wanafikiwa, na wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali kutanua soko la bidhaa za gesi kwa kutoa mikopo kwa waajiriwa kupitia maeneo wanayofanyia kazi, Aidha BI. MONICA amesema mbali ya kuwakopesha wafanyakazi bidhaa zao, wanatoa pia mikopo kwa watu wa kawaida ambao watalazimika kulipa kwa riba ya asilimia 18, na katika kuhakikisha vilevilke wanasaidia katika kupunguza tatizo la ajira kwa vijana kampuni ya ORYX imekuwa na utaratibu wa kuwakopesha vijana mitaji ili mradi wawe leseni ya biashara, mzani na eneo la kufanyia biashara. PEDWA ni chama cha waandishi wa habari za mazingira na za watu wenye ulemavu, kinacholenga kutumia tasnia ya habari kuwajuza wanajamii juu ya umuhimu wa kutunza mazingira kwa faida ya kizazi cha kesho. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA

MAMLAK YA MJI MDOGO MLANDIZI HOI.

WAZABUNI FEKIO CHANZO CHA KUZOROTA MAENDELEO.