Ben Komba/Pwani-Tanzania/Wednesday, April 11, 2012/.06:48:08 PM
Mama mmoja mkazi wa mjini Kibaha BI. DIGNA LAURENT MASHAKAhivi karibuni amekumbwa na kisanga cha kutelekezewa watoto na mali za familia kuuzwa na mume wake wa ndoa, kwa sababu ya ndoa yao kuingiliwa na Mama mmoja mjane mkristo wa TAG anayejulikana kwa jina la Mama BETTY ambaye awali alikuwa anadai ana undugu na Mume wa mlalamikaji lakini kumbe ni kinyume chake.
BI. DIGNA MASHAKA amebainisha mgogoro ulianza kwa yeye kuitwa mchawi na mume wake, na katika madai yake hayo siku moja mumewe BW. LAURENT MASHAKA (Michuzi) alirudi nyumbani na kumwita aende chumbani na mara alivyoingia akaanza kumkaba kiasi cha majirani kujitokeza na kuja kumuamulia, huku akidai ameweka uchawi kwenye viatu vyake na hivyo kumsababishia kupata fangasi.
Na kutokana na tukio hilo BI.DIGNA MASHAKA aliamua kufungua kesi ya dhidi ya mume wake akilalamikia kitendo kilichofanywa naye, na lengo sio kuachana na mumewe, lakini kesi hiyo iliendeshwa kwenye mahakama ya Mkuza na mumewe huyo kuonekana hana hatia. Wakati kesi hiyo ikiendelea naye mume akaenda katika mahakama ya mwanzo Maili moja kufungua shauri la kudaitalaka kutoka kwa mke wake ikiwa pamoja na kugawanya mali, ambapo mali zilizogawiwa zilikuwa za mke tu.
Mbali ya kufungua shauri hilo BW. MASHAKA aliuza nyumba mbili na kupora nyumba nyingine ambayo ipo katika kiwanja cha mtoto wa BI. DIGNA MASHAKA ambaye alizaa na mtu mwingine kabla ya kukutana na mume wake huyo waliyefunga naye ndoa mwaka 2009 na kiwanja kilinunuliwa mwaka 2008 na ni cha mtoto huyo anayejulikana kwa jina la GIFT.
Naye mtoto wa Baba huyo, BW. HUSSEIN MASHAKA amemlaani Mama BETTY ambaye mwanzoni alikuwa anajifanya ndugu ya Baba yao na kumchukulia kama ndugu kumbe ndio ambaye amewasbabishia matatizo ndani ya familia yao ya watoto watano, ingawa yeye sio mtoto wa mama huyo lakini amechoshwa na vitimbi anavyofanya Baba yao kiasi cha kuwafukuza nyumbani watoto wake kwa ya MAMA BETTY.
Wao kwa upande wao wanaiomba serikali kuzitupia macho kesi mbalimbali ambazo zimeshafunguliwa lakini zimekuwa zikisusua kiasi cha kutishi ustawi wa familia kutokana na muda mwingi kuutumia katika kufuatilia kesi, na huku watoto wakitangatanga klutokana na kukosa makazi kutokana baba huyo kuuza nyumba.
Juhudi za kumpata mama. BETTY kwa njia ya simu zilishindikana baada ya kupatikana mwanzo na kusema tuonane saa kumi, lakini baadaye alipopigiwa simu yake haikupatikana hewani, inasemekana mama huyo ni muumini wa Kanisa la TANZANIA ASSEMBLES OF GOD.
END.
Comments
Post a Comment