BAJETI YA HALMASHAURI WILAYA KIBAHA
Ben Komba/Pwani-Tanzania/Tuesday, 10 April, 2012/6:46:32 PM
Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2012/2013 halmashauri ya wilaya ya Kibaha imepanga kutumia jumla ya shilingi bilioni 14.8 ambapo kati ya fedha hizo ni shilingi bilioni 12 ndizo zitakazotoka serikali kuu.
Hayo yamesemekana katika kikao maalum cha bajeti cha baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Kibaha, wakati Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, BW. CHRISTOPHER MDUMA alipokuwa anawasilisha makisio na makadirio ya mapato na matumizi katika kipindi cha mwaka 2012/2013.
BW.MDUMA amesema kati ya fedha hizo ambazo zimeanishwa katika bajeti hiyo, shilingi bilioni 2.5 ikiwa ni makusanyo ya ndani na ikiwa pamoja na michango ya jamii na nguvukazi yao ikiwa zaidi ya shilingi bilioni 10.
BW. MDUMA akizungumzia upande wa mishahara amefafanua zaidi ya shilingi bilioni 8 zimetengwa upande huo, na matumizi ya kawaida yanakadiriwa kufikia shilingi bilioni 2.8 na miradi ya maendeleo ikiwa imetengewa shilingi bilioni 3.6.
Awali akiongea katika kikao hicho maalum cha Baraza la madiwani, mwenyekiti wa Baraza hilo, MH. MANSOOR KISABENGO amesema misingi ya kuandaliwa bajeti hii ni vipaumbele ambvyo vimneibuliwa na wananchi wenyewe katika maeneo yao.
Hivyo kwa kufuata miongozo iliyotolewa na serikali kuu pamoja na maagizo ya viongozi wa juu ambayo wameyatoa kufanikisha utekelezaji wa dira ya Taifa ya maendeleo ya 2025, na halmashauri itaendelea kutekeleza muda wa kati wa miaka mitano wa 2012/2013 na 2015/ 2016.
Ambapo MH. KISABENGO ameongeza kuwa malengo makuu yatakuwa utekelezaji wa vipaumbele vilivyoainishwa kwenye MKUKUTA II na maelekezo ya utekelezaji ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010-2015.
END.
Comments
Post a Comment