RIPOTI YA MTOTO ALIBAKWA YATHIBITISHA NDIVYO.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/4/1/2012 6:44:26 PM Taarifa ya daktari kuhusiana na tukio la kubakwa kwa mtoto wa mwenye umri wa miaka 3 na miezi minane ambalo limetokea March 27 mwaka huu imeshatolewa na kuthibitisha kuwa ni kweli mtoto huyto alifanyiwa kitendo hicho cha kikatili na kijana huyo ambaye anadaiwa kuwa na miaka zaidi ya 20. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mama wa mtoto huyo, BI. ASHURA WAZIR amesema majibu hayo ambayo yanafuatiwa uchunguzi uliofanyika katika Hospitali teule ya mkoa ya Tumbi. Na kwa mujibu wa vyeti hivyo ambavyo mwandishi wa habari hizi ameviona vinaonyesha kuwa mtoto huyo amekutwa na michubuko meneo ya siri, damu na mbegu mbichi za kiume zinaaokadiriwa gramu 1. Cheti hicho namba:MFM 40 na namba ya uandikishaji 004 kilichotolewa hospitali ya Tumbi, kimeonyesha pia dawa alizopewa mtoto baada ya msukosuko huo ni PANADOL, Akashauriwa kuogea DETTOL, Erythromycin na kutakiwa kuhudhuria kituo cha kupima UKIMWI na kumuona mganga bingwa wa magonjwa ya kinamama. Cheti hicho kinaonyesha siku mbili baada ya tukio nmtoto huyo alipatiwa dawa nyingine zikiwemo zile za kuzuia maambukizi ya UKIMWI, ya AZT, 3TC na NEVERAPINE. Mtuhumiwa wa tukio hilo aliyejulikana kwa jina moja JUSTIN ambaye wenyeji wake wanaficha ubini wa kijana yupo nje kwa dhamana. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA

MAMLAK YA MJI MDOGO MLANDIZI HOI.

VIDEO - CWT WACHAGUANA PWANI.