Posts

Showing posts from March, 2015

VIDEO-VIONGOZI WA DINI WATAKIWA WASIJIINGIZE KTK SIASA.

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/29/2015 3:52:58 PM Viongozi wa dini nchini wametakiwa kutojiingiza moja kwa moja kwenye siasa ili kuweza kufanya kazi sambamba serikalimkatika kuhakikisha hali ya amani na utulivu inadumu nchini. Mwangalizi wa makanisa ya PENTECOSTAL MISSION OF TANZANIA,Pastor GERVASE MASANJA ameongea hayo alipokutana na waandishi wa Habari   ofisini kwake amesema si vyema kwa viongozi wa dini kujiingiza katika mambo ya kisiasa kunaweza kuhatarisha amani na utulivu tulionao. Pastor MASANJA amechukua fursa hiyo kuwasisitiza wananchi kujitokeza kwenda kupiga kura katika mchakato wa kura ya maoni kuhusiana na katiba pendekezwa ili kupata fursa  ya kuweza kuhoji iwapo mambo yatakwenda ndivyo sivyo. Aidha amekemea tabia ya baadhi ya wanasiasa na viongozi kuwahamasisha wananchi kwenda kupiga kura kwa kufuata misimamo wanayofuata wao, jambo ambalo linakiuka dhamira ya msingi ya mtu binafsi. Ameongeza kuwa kufuatia kukabiliwa na chaguzi siku za usoni ni vyema

VIDEO-TUME YA MIPANGO OFISI RAIS WAPONGEZWA.

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/27/2015 4:46:36 PM Imesemekana mjini Kibaha kuwa mabaraza ya wafanyakazi ni vyombo muhimu katika kuongeza ufanisi wa  kazi ikiwa pamoja na kufanya maamuzi mbalimbali yanayohusu maslahi ya wafanyakazi,taasisi na Taifa kwa ujumla. Mkuu wa mkoa wa pwani, Mhandisi EVARIST NDIKILO ameyazungumza hayo wakati akifungua kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Rais,Tume ya mipango mjini Kibaha. Mhandisi NDIKILO amesema ni wajibu wa mabaraza haya kama vyombo vya ushauri na usimamizi katika kuhakikisha kuwa waajiri na watumishi wanatambua wajibu na haki zao na kuzingatia maadili ya utumishi wao ili kuleta matokeo makubwa ya utendaji kazi yenye tija, staha na upendo. Aidha mkuu huyo wa mkoa wa Pwani mhandisi NDIKILO amefafanua                kuwa hata kama kutakuwa na sera,sheria na kanuni nzuri za kazi katika eneo la kazi kama hakuna malengo ya pamoja na ushirikiano baina ya mwajiri na mwajiriwa ni vigumu taasisi hiyo kuwa na tija. Awali akizu

USHIRIKIANO KATI YA MWAJIRI NA MTUMISHI NI CHACHU KTK MAENDELEO TAASIS- RC NDIKILO

Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/27/2015 4:46:36 PM Imesemekana mjini Kibaha kuwa mabaraza ya wafanyakazi ni vyombo muhimu katika kuongeza ufanisi wa  kazi ikiwa pamoja na kufanya maamuzi mbalimbali yanayohusu maslahi ya wafanyakazi,taasisi na Taifa kwa ujumla. Mkuu wa mkoa wa pwani, Mhandisi EVARIST NDIKILO ameyazungumza hayo wakati akifungua kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Rais,Tume ya mipango mjini Kibaha. Mhandisi NDIKILO amesema ni wajibu wa mabaraza haya kama vyombo vya ushauri na usimamizi katika kuhakikisha kuwa waajiri na watumishi wanatambua wajibu na haki zao na kuzingatia maadili ya utumishi wao ili kuleta matokeo makubwa ya utendaji kazi yenye tija, staha na upendo. Aidha mkuu huyo wa mkoa wa Pwani mhandisi NDIKILO amefafanua                kuwa hata kama kutakuwa na sera,sheria na kanuni nzuri za kazi katika eneo la kazi kama hakuna malengo ya pamoja na ushirikiano baina ya mwajiri na mwajiriwa ni vigumu taasisi hiyo kuwa na tija. Awali akizungum

VIDEO-BAADA YA KUSUSWA WANANCHI WAJITOLEA KUJENGA BARABARA

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/26/2015 8:19 PM Wakazi wa mtaa wa Karabaka Kata ya Misugusugu katika halmashauri ya mji wa Kibaha wamekusanyana na kuamua kuchonga barabara kuelekea katika maeneo yao kufuatia maeneo yao kutokuwa na miundombinu ya barabara. Mwenyekiti ya serikali ya mtaa wa Karabaka, BW.IDD MSANGAZI amesema amewakusanya wakazi wa mtaa wake ili waweze kukabiliana na changamoto kubwa wanayokabiliana nayo ya ukosefu wa miundombinu ya barabara. BW.MSANGAZI amesema kuwa mtaa wake ni mmoja wa mitaa wenye nyumba za kisasa lakini zimejengwa bila kufuatilia utaratibu wa mipango miji na hivyo kusababisha baadhi ya watu watajikuta wanapata hasara itajkayosababishwa na kutowajibika kwa watu wa mipango miji. Amefafanua Kata ya Misugusugu ni moja ya Kata zilizopo katika mji wa Kibaha ambapo mpaka sasa katrika mtaa huo hakuna huduma muhimu  za kijamii kama maji,umem e na barabara. BW.MSANGAZI ameongeza kuwa yeye kwa kushirikiana na wananchi wa mtaa wake kwa njia ya m

KUENDEKEZA UVYAMA KWAATHIRI KAZI ZA KUJITOLEA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/26/2015 8:19 PM Wakazi wa mtaa wa Karabaka Kata ya Misugusugu katika halmashauri ya mji wa Kibaha wamekusanyana na kuamua kuchonga barabara kuelekea katika maeneo yao kufuatia maeneo yao kutokuwa na miundombinu ya barabara. Mwenyekiti ya serikali ya mtaa wa Karabaka, BW.IDD MSANGAZI amesema amewakusanya wakazi wa mtaa wake ili waweze kukabiliana na changamoto kubwa wanayokabiliana nayo ya ukosefu wa miundombinu ya barabara. BW.MSANGAZI amesema kuwa mtaa wake ni mmoja wa mitaa wenye nyumba za kisasa lakini zimejengwa bila kufuatilia utaratibu wa mipango miji na hivyo kusababisha baadhi ya watu watajikuta wanapata hasara itajkayosababishwa na kutowajibika kwa watu wa mipango miji. Amefafanua Kata ya Misugusugu ni moja ya Kata zilizopo katika mji wa Kibaha ambapo mpaka sasa katrika mtaa huo hakuna huduma muhimu  za kijamii kama maji,umem e na barabara. BW.MSANGAZI ameongeza kuwa yeye kwa kushirikiana na wananchi wa mtaa wake kwa njia ya mic

VIDEO+UMWAGILIAJI WA DRIPU MKOMBOZI KILIMO CHA MBOGAMBOGA

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/24/2015 9:36:18 PM Wakulima wa mbogamboga nchini wametakiwa kulima kilimo kitakachotumia maji ya wastani ili kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa maji ya kutosha katika kukidhi mahitaji ya bidhaa hiyo. Mtaalamu wa kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia njia ya unyunyuizaji ambayo ni maarufu nchini Israel inayojulikana kama DRIP IRRIGATION SYSTEM , BW.EPHRAHIM MASSAWE amesema kwa kufanya hivyo wataweza kukabiliana na changamoto kubwa ya ukosefu wa maji kwa ajili ya umwagiliaji. BW.MASSAWE amebainisha kuwa iwapo wakulima wa mbogamboga watatumia mbinu ya umwagiliaji wa kunyunyiza wataweza kutumia maji machache wanayopata kwa manufaa na tija kubwa, kwani mazao yatastawi na kuweza kupata mavuno makubwa. Mtaalamu huyo amewasisitizia wakulima wote wa mbogamboga wanaotegemea shughuli hiyo kuendesha maisha yao ya kila siku kutosita kubadilika na kutumia mbinu mpya za umwagiliaji ambao utarahisisha upatikanaji wa maji kwani badala ya kutumia maji men

WAKULIMA WA MBOGA WATAKIWA KUTUMIA UMWAGILIAJI WA KUNYUNYIZA, ISRAEL IRRIGATION SYSTEM.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/24/2015 9:36:18 PM Wakulima wa mbogamboga nchini wametakiwa kulima kilimo kitakachotumia maji ya wastani ili kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa maji ya kutosha katika kukidhi mahitaji ya bidhaa hiyo. Mtaalamu wa kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia njia ya unyunyuizaji ambayo ni maarufu nchini Israel inayojulikana kama DRIP IRRIGATION SYSTEM , BW.EPHRAHIM MASSAWE amesema kwa kufanya hivyo wataweza kukabiliana na changamoto kubwa ya ukosefu wa maji kwa ajili ya umwagiliaji. BW.MASSAWE amebainisha kuwa iwapo wakulima wa mbogamboga watatumia mbinu ya umwagiliaji wa kunyunyiza wataweza kutumia maji machache wanayopata kwa manufaa na tija kubwa, kwani mazao yatastawi na kuweza kupata mavuno makubwa. Mtaalamu huyo amewasisitizia wakulima wote wa mbogamboga wanaotegemea shughuli hiyo kuendesha maisha yao ya kila siku kutosita kubadilika na kutumia mbinu mpya za umwagiliaji ambao utarahisisha upatikanaji wa maji kwani badala ya kutumia maji mengi

VIDEO=MKUU WA MKOA WA PWANI AWAHAKIKISHIA WANANCHI MAJI.

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/22/2015 4:38:44 PM Mkuu wa mkoa wa Pwani,BW.EVARIST NDIKILO amewahakikishia wananchi wa kijiji cha Lupunga Kata ya Ruvu stesheni wilayani Kibaha kwamba mradi wa maji utakaofaidisha vijiji 10 katika halmashauri ya wilaya Kibaha na hivyo kupunguza kero kubwaya maji  inayowakabili wakazi wa vijiji hivyo. Mkuu huyo mpya wa mkoa wa  Pwani, Mhandisi EVARIST NDIKILO ameyazungumza hayo wakati wa maadhimisho ya wiki ya maji yaliyoanza Machi 16 na kilelee chake Machi 22, ambayo yamefanyika kimkoa wilayani Kibaha katika kijiji cha Lupunga. Ambapo Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi NDIKILO amewahaki9kishia wakazi hao wa vijiji 10 ambavyo vitafaidika na mradi huo uliogharimu shilingi Milioni 250, kuwa yeye kwa kushirikiana watendaji wengine watashirikiana kutafuta njia ya haraka ya kukamilisha mradi huo unaokwama kutokana na kukosekana kwa umeme. Mhandisi NDIKILO amongeza kuwa moja ya hatua ambayo ataichukua ni kukaa pamoja na shirika la umeme mkoa wa P

MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI YAGUBUKWA NA MVUA TELE.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/22/2015 4:38:44 PM Mkuu wa mkoa wa Pwani,BW.EVARIST NDIKILO amewahakikishia wananchi wa kijiji cha Lupunga Kata ya Ruvu stesheni wilayani Kibaha kwamba mradi wa maji utakaofaidisha vijiji 10 katika halmashauri ya wilaya Kibaha na hivyo kupunguza kero kubwaya maji  inayowakabili wakazi wa vijiji hivyo. Mkuu huyo mpya wa mkoa wa  Pwani, Mhandisi EVARIST NDIKILO ameyazungumza hayo wakati wa maadhimisho ya wiki ya maji yaliyoanza Machi 16 na kilelee chake Machi 22, ambayo yamefanyika kimkoa wilayani Kibaha katika kijiji cha Lupunga. Ambapo Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi NDIKILO amewahaki9kishia wakazi hao wa vijiji 10 ambavyo vitafaidika na mradi huo uliogharimu shilingi Milioni 250, kuwa yeye kwa kushirikiana watendaji wengine watashirikiana kutafuta njia ya haraka ya kukamilisha mradi huo unaokwama kutokana na kukosekana kwa umeme. Mhandisi NDIKILO amongeza kuwa moja ya hatua ambayo ataichukua ni kukaa pamoja na shirika la umeme mkoa wa Pwani

MAANDALIZI YA MEI MOSI YAPAMBA MOTO PWANI_VIDEO

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/21/2015 8:57:58 PM Maandalizi ya sikukuu ya wafanyakazi mkoa wa Pwani yameanza ambayo mwaka huu kimkoa yatafanika wilayani Mafia chini ya usimamizi wa chama cha wahifadhi,mahoteli na nyumba za kulala wageni. Mwenyekiti  wa CHODAWU Mkoa wa PWANI, BW.PIUS MSILU amesema mwaka huu maadhimisho hayo yanafanyika wilayani Mafia ili kutoa fursa kwa wafanyakazi kisiwani humo kushiriki kikamilifu sherehe hizo na kuweza kuweka bayana changamoto mbalimbali zinazowakabili. BW.MSILU ameongeza kuwa wamejipanga kuhakikisha wanawasiliana na waajiri na wadau wengine katika kuhakikisha wanapata fedha za kutosha kufanikisha maadhimisho hayo. Ameongeza kuwa ni wajibu wa waajiri kuwasilisha majina ya wafanyakazi bora ili waweze kupatiwa zawadi wanazostahili, ameongeza kuwa CHODAWU imepata mafanikio mbalimbali kwa kuwasaidia wafanyakazi wanachama wa chama hicho kupata haki zao msingi. Naye mjumbe wa CHODAWU kutoka Wilayani Mafia BW.CLEVER MWAIKAMBO amewata

MAANDALIZI YA MEI MOSI YAPAMBA MOTO PWANI.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/21/2015 8:57:58 PM Maandalizi ya sikukuu ya wafanyakazi mkoa wa Pwani yameanza ambayo mwaka huu kimkoa yatafanika wilayani Mafia chini ya usimamizi wa chama cha wahifadhi,mahoteli na nyumba za kulala wageni. Mwenyekiti  wa CHODAWU Mkoa wa PWANI, BW.PIUS MSILU amesema mwaka huu maadhimisho hayo yanafanyika wilayani Mafia ili kutoa fursa kwa wafanyakazi kisiwani humo kushiriki kikamilifu sherehe hizo na kuweza kuweka bayana changamoto mbalimbali zinazowakabili. BW.MSILU ameongeza kuwa wamejipanga kuhakikisha wanawasiliana na waajiri na wadau wengine katika kuhakikisha wanapata fedha za kutosha kufanikisha maadhimisho hayo. Ameongeza kuwa ni wajibu wa waajiri kuwasilisha majina ya wafanyakazi bora ili waweze kupatiwa zawadi wanazostahili, ameongeza kuwa CHODAWU imepata mafanikio mbalimbali kwa kuwasaidia wafanyakazi wanachama wa chama hicho kupata haki zao msingi. Naye mjumbe wa CHODAWU kutoka Wilayani Mafia BW.CLEVER MWAIKAMBO amewataka

VIDEO- VYAMA VYATAKIWA KUHAKIKI KATIBA KUEPUKA KUWA TOFAUTI NA KATIBA YA NCHI.

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/19/2015 8:51:58 PM Vyama vya siasa nchini vimetakiwa kupitia katiba zao na kuzihakiki ili kutoenda kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika suala zima la kuzingatia haki za msingi za binadamu. Katibu wa ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPARENT  mkoa wa Pwani, BW.MRISHO HALFAN SWAGALA amesema hayo kufuatia hatua ya baadhi ya vyama vya siasa kutunga katiba ambayo inamzuia mwanachama kwenda mahakamani  anapoona haki yake inakiukwa. BW.SWAGALA amesema kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa haki ya mtu anapoona haki yake inapindishwa anaruhusiwa kwenda mahakamani, Lakini cha kushangaza kuna baadhi ya vyama vya siasa zina katiba ambayo inakatazan mwanachama wake kwenda mahakamani hata an apoonewa. Amefafanua Katibu huyo wa ACT Mkoa wa Pwani, BW.MRISHO HALFAN SWAGALA  kuwa iwapo katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inaruhusu kwa mwananchi akashitaki mahakamani iwapo anaona haki yake inakiukwa, basi ni

KATIBA ZA VYAMA ZISIKIUKE KATIBA YA NCHI-ACT

Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/19/2015 8:51:58 PM Vyama vya siasa nchini vimetakiwa kupitia katiba zao na kuzihakiki ili kutoenda kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika suala zima la kuzingatia haki za msingi za binadamu. Katibu wa ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPARENT  mkoa wa Pwani, BW.MRISHO HALFAN SWAGALA amesema hayo kufuatia hatua ya baadhi ya vyama vya siasa kutunga katiba ambayo inamzuia mwanachama kwenda mahakamani  anapoona haki yake inakiukwa. BW.SWAGALA amesema kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa haki ya mtu anapoona haki yake inapindishwa anaruhusiwa kwenda mahakamani, Lakini cha kushangaza kuna baadhi ya vyama vya siasa zina katiba ambayo inakatazan mwanachama wake kwenda mahakamani hata an apoonewa. Amefafanua Katibu huyo wa ACT Mkoa wa Pwani, BW.MRISHO HALFAN SWAGALA  kuwa iwapo katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inaruhusu kwa mwananchi akashitaki mahakamani iwapo anaona haki yake inakiukwa, basi ni vyem

VIDEO-MIZENGWE KUELEKEA UCHAGUZI MKUU KIBAHA MJINI,

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/17/2015 7:59:49 PM Kufuatia ushindi wa kwikwi waliopata chama cha mapinduzi katika uchaguzi wa serikali za mitaa mjini Kibaha, chama hicho kimemsimamisha Katibu mwenezi wa chama hicho kata ya Mailimoja BW.LAZARO KULIGWA kwa sababu mbalimbali. Akiongea na mwandishi wa Habari hizi, BW.KULIGWA ameshangazwa na hatua iliyochukuliwa na mkutano wa kamati ya utekelezaji ya Kata ya kuamua kumuengua kwa muda kutoka katika nafasi yake ya kuchaguliwa. BW.KULIGWA ameonggeza kuwa mara baada ya kukamilika mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa ndipo mizengwe ilipoanza kutokana na uwepo wa kambi zinazopingana kuwania ubunge wa Jimbo la Kibaha mjini. Na kutokana na hilo kumekuwepo na wanachama wa CCM ambao wanatumia muda huu kuelekea uchaguzi kufanya fitna na majungu  ambayo yanahatarisha amani na mshikamano katika chama. BW.KULIGWA amewataka wanachama wanaowania nafasi ya ubunge katika Jimbo la uchaguzi Kibaha mjini kuwa macho na baadhi watu wanaow

WATANZANIA WATAKIWA KUWA MACHO NA MBEGU ZILIZOBADILISHWA VINASABA-VIDEO.

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/15/2015 4:47:04 PM Watanzania wametakiwa kutilia mkazo ufugaji na kilimo cha asili ili kuepuka kutumbukia katika mtego wa kujikuta wa natumia mbegu ambazo zimebadilishwa vinasaba na hivyo kuhatarisha afya ya mlaji. Akizungumza na mwandishi wa Habari hizi, mtaalamu wa masuala ya kilimo anayetambulika kimataifa, BW.EPHRAHI MASSAWE ambaye anamiliki shamba la mfano katika makazi yake yaliyopo Kibaha kwa  Mfipa katika halmashauri ya mji wa Kibaha, iwapo wananchi wakifuata maelekezo ya kitaalamu juu ya kilimo na ufugaji kuna uwezekano mkubwa wa kupunguza makali ya maisha. BW.MASSAWE ambaye ni mwakilishi wa kampuni ya madawa ya Ufaransa inayojulikana kama LAPROVET, Amebainisha kitu kilichomsukuma kuanzisha shamba darasa kutokana na kila mtu kutojua nini wafanye ili kuongeza mapato ya kilimo na mifugo. Ameongeza kuwa anachotaka kuwafundisha wagani,wataalamu wa kilimo na mifugo pamoja na wakulima na wafugaji wa kawaida kwa kuwapa uzoefu wa kimataifa

JAMII YATAKIWA KUTUNZA MITI DAWA,---VIDEO

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/12/2015 5:26:29 PM Uharibifu wa mazingira na ukataji wa miti ovyo kumesababisha kuadimika kwa miti dawa ya kutosha kuweza kukabiliana na magonjwa ambayo yanatibika kwa kutumia tiba za jadi kupitia misitu tuliyonayo. Mtaalam wa Tiba za jadi mkazi wa Miono wilayani Bagamoyo katika mkoa wa Pwani, BW.JUMA NASSORO MTEGETA ambaye pia ni mtaalamu wa kucheza na Nyoka, amebainisha kuwa changamoto za maisha ya kisasa ikiwemo uuzaji holela wa ardhi kunakofanywa na viongozi wa vijiji kwa tamaa ya fedha kunaathiri kwa kiasi kikubwa jamii kutokana na miti dawa mingi kukatwa. Bw. NASSORO amebainisha kuwa kati ya sababu kubwa ni viongozi kuuza ardhi yote bila kufikiria kuacha hifadhi yam situ wa kijiji, kwa ajili ya matumizi mengine ya wanadamu kama kuokota kuni, kutafuta miti dawa kwa ajili ya matumizi ya tiba. Aidha BW. NASSORO ameongeza kuwa mbaya zaidi kumekuwepo na ushirikishaji mdogo wa wananchi linapokuja suala la kuuza ardhi kwa wageni na uamuzi h

MSIBA WA MWANAMKE KONDAKTA WA DALADALA- VIDEO.

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/10/2015 Mamia ya wakazi wa Kibamba wamekutwa wamekusanyika katika chumba ha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Tumbi katika mkoa wa Pwani, kushuhudia kuagwa kwa mwanadada jasiri BI.MARY PASCHAL. Mwanadada huyo ambaye enzi ya uhai wake alikuwa kondakta wa gari zinazosafirisha abiria kati ya Ubungo na Kibaha, alipatwa na mauti hayo eneo la Mbezi akiwa kazini baada gari aina ya NOAH kuigonga HIACE aliyokuwa anafanyia kazi. Kwa mujibu wa mashuhuda marehemu katika kipindi hicho alikuwa amekaa katika kiti cha wanafunzi na huku akiendelea kuita abiria kama ilivyo ada kwa makondakta na ndipo ilipotokea na kugonga ubavuni gari yao nay eye kudondokea mtarani na tairi ya nyuma ya gari ikamkanyaga maeneo ya kwenye nyonga Mwili marehemu MARY PASCHAL umesafirishwa kwenda WILAYANI Kondoa Mkoani Dodoma kwa ajili ya mazishi na ameacha watoto wawili mmoja wa darasa la tatu na mwingine mwanafunzi wa kidato cha pili waliokuwa wanamtegemea. END.

HATIMAYE ILE SHULE MBOVU YAPATA MSAADA-VIDEO.

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/9/2015 9:21:20 PM Mbunge wa Kibaha mjini,Mheshimiwa SYLVESTER KOKA amekabidhi mabati 50 na mifuko 50 ya saruji kwa shule ya msingi Maili moja yenye thamani ya shilingi milioni 4  laki 7 katika suala zima la kukabiliana na uchakavu mkubwa wa majengo uliopo shuleni hapo. Akikabidhi msaada huo, Mbunge huyo wa Kibaha mjini, Mheshimiwa KOKA amebainisha kuwa wakati sasa umefika kuhakikisha kunakuwepo na ushirikiano kati ya walimu na wazazi ili kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu. Mheshimiwa KOKA ameongeza kuwa kumlea mwanafunzi si suala la Mwalimu peke yake bali linahitaji ushirikiano madhubuti kati ya wanafunzi,wazazi na walimu. Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mailimoja, BW.REGINALD FANUEL amemshukuru mbunge pamoja na wadau wengine ambao kwa njia moja au nyingine wamechangia kwa hali na mali kufanikisha kupatikana vifaa vya ujenzi kwa ajili ya uimarishaji miundo mbinu ya majengo shuleni hapo. END.