VIDEO=MKUU WA MKOA WA PWANI AWAHAKIKISHIA WANANCHI MAJI.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/3/22/2015 4:38:44 PM
Mkuu wa mkoa
wa Pwani,BW.EVARIST NDIKILO amewahakikishia wananchi wa kijiji cha Lupunga Kata
ya Ruvu stesheni wilayani Kibaha kwamba mradi wa maji utakaofaidisha vijiji 10
katika halmashauri ya wilaya Kibaha na hivyo kupunguza kero kubwaya maji inayowakabili wakazi wa vijiji hivyo.
Mkuu huyo
mpya wa mkoa wa Pwani, Mhandisi EVARIST
NDIKILO ameyazungumza hayo wakati wa maadhimisho ya wiki ya maji yaliyoanza
Machi 16 na kilelee chake Machi 22, ambayo yamefanyika kimkoa wilayani Kibaha
katika kijiji cha Lupunga.
Ambapo Mkuu
wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi NDIKILO amewahaki9kishia wakazi hao wa vijiji 10
ambavyo vitafaidika na mradi huo uliogharimu shilingi Milioni 250, kuwa yeye
kwa kushirikiana watendaji wengine watashirikiana kutafuta njia ya haraka ya
kukamilisha mradi huo unaokwama kutokana na kukosekana kwa umeme.
Mhandisi
NDIKILO amongeza kuwa moja ya hatua ambayo ataichukua ni kukaa pamoja na
shirika la umeme mkoa wa Pwani kuangalia nini kinafanyika ili mradi huo ambao
umegharimu mamilioni ya fedha kuhakikisha mradi huo unaanza kunufaisha wananchi
wa vijiji hivyo.
Kaimu katibu
tawala msaidizi maji, BW.CECIL SIAFU,
akisoma taarifa ya maji na mazingira ya mkoa wa Pwani ambayo imetolewa
katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji katika kijiji cha Lupunga amesema
pamoja na jitihada za mkoa katika kufanikisha upatikanaji wa maji safi na kuna
changamoto mbalimbali zinajitokeza.
BW.SIAFU
amebainisha kuwa changamoto hizo ni pamoja na kuchelewa kupata fdha za ujenzi
wa miundombinu ya maji kutoka kwa wafadhili pamoja na wizara ya maji.
Changamoto
nyingine ni wakandarasi wengi wamekuwa na mitaji midogo kutokana na miradi
mingi wanayotekeleza kuwa ni miradi midogo kutokana na gharama zake nkuwa kati
ya milioni 200 na milioni 500 na hivyo ushinwa kuendelea na kazi wanapokosa
malipoo hata kwa muda mfupi.
END
Comments
Post a Comment