MAANDALIZI YA MEI MOSI YAPAMBA MOTO PWANI_VIDEO
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/3/21/2015 8:57:58 PM
Maandalizi ya
sikukuu ya wafanyakazi mkoa wa Pwani yameanza ambayo mwaka huu kimkoa
yatafanika wilayani Mafia chini ya usimamizi wa chama cha wahifadhi,mahoteli na
nyumba za kulala wageni.
Mwenyekiti wa CHODAWU Mkoa wa PWANI, BW.PIUS MSILU
amesema mwaka huu maadhimisho hayo yanafanyika wilayani Mafia ili kutoa fursa
kwa wafanyakazi kisiwani humo kushiriki kikamilifu sherehe hizo na kuweza
kuweka bayana changamoto mbalimbali zinazowakabili.
BW.MSILU
ameongeza kuwa wamejipanga kuhakikisha wanawasiliana na waajiri na wadau
wengine katika kuhakikisha wanapata fedha za kutosha kufanikisha maadhimisho
hayo.
Ameongeza kuwa
ni wajibu wa waajiri kuwasilisha majina ya wafanyakazi bora ili waweze kupatiwa
zawadi wanazostahili, ameongeza kuwa CHODAWU imepata mafanikio mbalimbali kwa
kuwasaidia wafanyakazi wanachama wa chama hicho kupata haki zao msingi.
Naye mjumbe
wa CHODAWU kutoka Wilayani Mafia BW.CLEVER MWAIKAMBO amewataka watu wote
watakaoshiriki maadhimisho hayo kutumia fursa hiyo kuja kuyafahamu mazingira ya
kuvutia ya kisiwa hicho chenye utajiri mkubwa mazao ya bahari.
END.
Comments
Post a Comment