KATIBA ZA VYAMA ZISIKIUKE KATIBA YA NCHI-ACT


Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/19/2015 8:51:58 PM
Vyama vya siasa nchini vimetakiwa kupitia katiba zao na kuzihakiki ili kutoenda kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika suala zima la kuzingatia haki za msingi za binadamu.

Katibu wa ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPARENT  mkoa wa Pwani, BW.MRISHO HALFAN SWAGALA amesema hayo kufuatia hatua ya baadhi ya vyama vya siasa kutunga katiba ambayo inamzuia mwanachama kwenda mahakamani  anapoona haki yake inakiukwa.

BW.SWAGALA amesema kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa haki ya mtu anapoona haki yake inapindishwa anaruhusiwa kwenda mahakamani, Lakini cha kushangaza kuna baadhi ya vyama vya siasa zina katiba ambayo inakatazan mwanachama wake kwenda mahakamani hata an apoonewa.

Amefafanua Katibu huyo wa ACT Mkoa wa Pwani, BW.MRISHO HALFAN SWAGALA  kuwa iwapo katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inaruhusu kwa mwananchi akashitaki mahakamani iwapo anaona haki yake inakiukwa, basi ni vyema vyama zikapitia upya ili kuepuka migogoro siku za usoni.

EN

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA