KUENDEKEZA UVYAMA KWAATHIRI KAZI ZA KUJITOLEA
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/3/26/2015 8:19 PM
Wakazi wa
mtaa wa Karabaka Kata ya Misugusugu katika halmashauri ya mji wa Kibaha
wamekusanyana na kuamua kuchonga barabara kuelekea katika maeneo yao kufuatia
maeneo yao kutokuwa na miundombinu ya barabara.
Mwenyekiti ya
serikali ya mtaa wa Karabaka, BW.IDD MSANGAZI amesema amewakusanya wakazi wa
mtaa wake ili waweze kukabiliana na changamoto kubwa wanayokabiliana nayo ya
ukosefu wa miundombinu ya barabara.
BW.MSANGAZI
amesema kuwa mtaa wake ni mmoja wa mitaa wenye nyumba za kisasa lakini
zimejengwa bila kufuatilia utaratibu wa mipango miji na hivyo kusababisha
baadhi ya watu watajikuta wanapata hasara itajkayosababishwa na kutowajibika
kwa watu wa mipango miji.
Amefafanua Kata
ya Misugusugu ni moja ya Kata zilizopo katika mji wa Kibaha ambapo mpaka sasa
katrika mtaa huo hakuna huduma muhimu za
kijamii kama maji,umem e na barabara.
BW.MSANGAZI
ameongeza kuwa yeye kwa kushirikiana na wananchi wa mtaa wake kwa njia ya
michango ya fedha na nguvukazi wameamua kwa pamoja kutoisubiri serikali kuja
kuwafanyia kila kitu na kuitaka kuchangia eneo ambalo wananchi wameibua mradi
wa maendeleo.
Aidha Mwenyekiti
huyo wa serikali ya mtaa wa KARABAKA kupitia tiketi ya CHADEMA, amewataka
wananchi kuacha kuingiza itikadi za kisiasa katika masuala yanayohusu maendeleo
na kama uchaguzi umeshapita na inabidi
kjila mtu akubali matokeo, na kushirikiana kama wananchi wan chi mojha
kuliletea taifa letu maendeleo.END
Comments
Post a Comment