VIDEO-TUME YA MIPANGO OFISI RAIS WAPONGEZWA.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/3/27/2015 4:46:36 PM
Imesemekana
mjini Kibaha kuwa mabaraza ya wafanyakazi ni vyombo muhimu katika kuongeza
ufanisi wa kazi ikiwa pamoja na kufanya
maamuzi mbalimbali yanayohusu maslahi ya wafanyakazi,taasisi na Taifa kwa
ujumla.
Mkuu wa mkoa
wa pwani, Mhandisi EVARIST NDIKILO ameyazungumza hayo wakati akifungua kikao
cha Baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Rais,Tume ya mipango mjini Kibaha.
Mhandisi
NDIKILO amesema ni wajibu wa mabaraza haya kama vyombo vya ushauri na usimamizi
katika kuhakikisha kuwa waajiri na watumishi wanatambua wajibu na haki zao na
kuzingatia maadili ya utumishi wao ili kuleta matokeo makubwa ya utendaji kazi
yenye tija, staha na upendo.
Aidha mkuu
huyo wa mkoa wa Pwani mhandisi NDIKILO amefafanua kuwa hata kama kutakuwa na sera,sheria
na kanuni nzuri za kazi katika eneo la kazi kama hakuna malengo ya pamoja na
ushirikiano baina ya mwajiri na mwajiriwa ni vigumu taasisi hiyo kuwa na tija.
Awali
akizungumza katika mkikao hicho, Kaimu Katibu mtendaji, Tume ya mipango ofisi
ya Rais, BIBI.FLORENCE MWANRI amesema tume ya mipango imeshakamilisha kuandaa
mwongozo wa usimamizi wa uwekezaji wa umma, ikiwa pamoja na kukamilisha tafiti
mbalimbali zinazolenga katika kuharakisha maendeleo ya ukuaji wa uchumi wan chi
yetu na mahitaji ya kufikia malengo ya dira ya Taifa ya maendeleo ya mwaka
2025.
END.
Comments
Post a Comment