VIDEO-MIZENGWE KUELEKEA UCHAGUZI MKUU KIBAHA MJINI,
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/3/17/2015 7:59:49 PM
Kufuatia ushindi
wa kwikwi waliopata chama cha mapinduzi katika uchaguzi wa serikali za mitaa
mjini Kibaha, chama hicho kimemsimamisha Katibu mwenezi wa chama hicho kata ya
Mailimoja BW.LAZARO KULIGWA kwa sababu mbalimbali.
Akiongea na
mwandishi wa Habari hizi, BW.KULIGWA ameshangazwa na hatua iliyochukuliwa na
mkutano wa kamati ya utekelezaji ya Kata ya kuamua kumuengua kwa muda kutoka
katika nafasi yake ya kuchaguliwa.
BW.KULIGWA
ameonggeza kuwa mara baada ya kukamilika mchakato wa uchaguzi wa serikali za
mitaa ndipo mizengwe ilipoanza kutokana na uwepo wa kambi zinazopingana kuwania
ubunge wa Jimbo la Kibaha mjini.
Na kutokana
na hilo kumekuwepo na wanachama wa CCM ambao wanatumia muda huu kuelekea
uchaguzi kufanya fitna na majungu ambayo
yanahatarisha amani na mshikamano katika chama.
BW.KULIGWA
amewataka wanachama wanaowania nafasi ya ubunge katika Jimbo la uchaguzi Kibaha
mjini kuwa macho na baadhi watu wanaowatumia kuganja njaa, kwa kutunga maneno
ya kwenda kuelezea wenye nia ya kugombea na kupatiwa vijisenti.
END
Comments
Post a Comment