VIDEO+UMWAGILIAJI WA DRIPU MKOMBOZI KILIMO CHA MBOGAMBOGA
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/3/24/2015 9:36:18 PM
Wakulima wa
mbogamboga nchini wametakiwa kulima kilimo kitakachotumia maji ya wastani ili
kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa maji ya kutosha katika kukidhi mahitaji
ya bidhaa hiyo.
Mtaalamu wa
kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia njia ya unyunyuizaji ambayo ni maarufu
nchini Israel inayojulikana kama DRIP IRRIGATION SYSTEM , BW.EPHRAHIM MASSAWE
amesema kwa kufanya hivyo wataweza kukabiliana na changamoto kubwa ya ukosefu
wa maji kwa ajili ya umwagiliaji.
BW.MASSAWE
amebainisha kuwa iwapo wakulima wa mbogamboga watatumia mbinu ya umwagiliaji wa
kunyunyiza wataweza kutumia maji machache wanayopata kwa manufaa na tija kubwa,
kwani mazao yatastawi na kuweza kupata mavuno makubwa.
Mtaalamu
huyo amewasisitizia wakulima wote wa mbogamboga wanaotegemea shughuli hiyo
kuendesha maisha yao ya kila siku kutosita kubadilika na kutumia mbinu mpya za
umwagiliaji ambao utarahisisha upatikanaji wa maji kwani badala ya kutumia maji
mengi kulowesha tuta zima la mboga, teknolojia hiyo nitatoa maji hayo kwenda
moja kwa moja katika mmea husika.
Teknolojia
hiyo ya umwagiliaji imetokea nchini Israel ambapo imetumika na inaendelea
kutumika katika uzalishaji wa kilimo cha matunda katika eneo ambalo awali
lilikuwa jangwa.
END.
Comments
Post a Comment