JAMII YATAKIWA KUTUNZA MITI DAWA,---VIDEO
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/3/12/2015 5:26:29 PM
Uharibifu wa
mazingira na ukataji wa miti ovyo kumesababisha kuadimika kwa miti dawa ya
kutosha kuweza kukabiliana na magonjwa ambayo yanatibika kwa kutumia tiba za
jadi kupitia misitu tuliyonayo.
Mtaalam wa
Tiba za jadi mkazi wa Miono wilayani Bagamoyo katika mkoa wa Pwani, BW.JUMA
NASSORO MTEGETA ambaye pia ni mtaalamu wa kucheza na Nyoka, amebainisha kuwa
changamoto za maisha ya kisasa ikiwemo uuzaji holela wa ardhi kunakofanywa na
viongozi wa vijiji kwa tamaa ya fedha kunaathiri kwa kiasi kikubwa jamii
kutokana na miti dawa mingi kukatwa.
Bw. NASSORO
amebainisha kuwa kati ya sababu kubwa ni viongozi kuuza ardhi yote bila
kufikiria kuacha hifadhi yam situ wa kijiji, kwa ajili ya matumizi mengine ya
wanadamu kama kuokota kuni, kutafuta miti dawa kwa ajili ya matumizi ya tiba.
Aidha BW.
NASSORO ameongeza kuwa mbaya zaidi kumekuwepo na ushirikishaji mdogo wa
wananchi linapokuja suala la kuuza ardhi kwa wageni na uamuzi hutolewa na watu
wane tu bila kufuata taratibu za kufuata vikao vinavyoshirikisha jamii yoyote
ili kukubaliana na uuzaji wowote wa ardhi mkubwa.
BW.NASSORO
amekemea tabia ya bbadhi ya viungo vya binadamu kufanya kazi zao na hivyo kumua
kuwauwa binadamu wenzao kwa kuwa tu ni Albino na kukiita kitendo hicho kama ni
unyama wa hali ya juu na kuitaka serikali ichukue hatua za haraka kukomesha
vitendo hivyo vinavyotishia uhai wa walemavu wa ngozi.
END
Comments
Post a Comment