WATANZANIA WATAKIWA KUWA MACHO NA MBEGU ZILIZOBADILISHWA VINASABA-VIDEO.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/15/2015 4:47:04 PM
Watanzania wametakiwa kutilia mkazo ufugaji na kilimo cha asili ili kuepuka kutumbukia katika mtego wa kujikuta wa natumia mbegu ambazo zimebadilishwa vinasaba na hivyo kuhatarisha afya ya mlaji.

Akizungumza na mwandishi wa Habari hizi, mtaalamu wa masuala ya kilimo anayetambulika kimataifa, BW.EPHRAHI MASSAWE ambaye anamiliki shamba la mfano katika makazi yake yaliyopo Kibaha kwa  Mfipa katika halmashauri ya mji wa Kibaha, iwapo wananchi wakifuata maelekezo ya kitaalamu juu ya kilimo na ufugaji kuna uwezekano mkubwa wa kupunguza makali ya maisha.

BW.MASSAWE ambaye ni mwakilishi wa kampuni ya madawa ya Ufaransa inayojulikana kama LAPROVET, Amebainisha kitu kilichomsukuma kuanzisha shamba darasa kutokana na kila mtu kutojua nini wafanye ili kuongeza mapato ya kilimo na mifugo.

Ameongeza kuwa anachotaka kuwafundisha wagani,wataalamu wa kilimo na mifugo pamoja na wakulima na wafugaji wa kawaida kwa kuwapa uzoefu wa kimataifa kupitia  mpango maalum ulioandaliwa na shirika la chakula ulimwenguni-FAO-

BW.MASSAWE ameongeza kuwa amekuwa akitoa kipaumbele kwa matumizi ya madawa ya asili katika kupambana na magonjwa mbalimbali kwa kutumia mti mwarubaini ambapo inampasa mtumiaji kuyasaga majani yake na mashine maalum na baadye kutumika kama dawa dhidi ya wadudu waharibifu wa mbogamboga.

END.



Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA