VIDEO-VIONGOZI WA DINI WATAKIWA WASIJIINGIZE KTK SIASA.



Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/29/2015 3:52:58 PM
Viongozi wa dini nchini wametakiwa kutojiingiza moja kwa moja kwenye siasa ili kuweza kufanya kazi sambamba serikalimkatika kuhakikisha hali ya amani na utulivu inadumu nchini.

Mwangalizi wa makanisa ya PENTECOSTAL MISSION OF TANZANIA,Pastor GERVASE MASANJA ameongea hayo alipokutana na waandishi wa Habari   ofisini kwake amesema si vyema kwa viongozi wa dini kujiingiza katika mambo ya kisiasa kunaweza kuhatarisha amani na utulivu tulionao.

Pastor MASANJA amechukua fursa hiyo kuwasisitiza wananchi kujitokeza kwenda kupiga kura katika mchakato wa kura ya maoni kuhusiana na katiba pendekezwa ili kupata fursa  ya kuweza kuhoji iwapo mambo yatakwenda ndivyo sivyo.

Aidha amekemea tabia ya baadhi ya wanasiasa na viongozi kuwahamasisha wananchi kwenda kupiga kura kwa kufuata misimamo wanayofuata wao, jambo ambalo linakiuka dhamira ya msingi ya mtu binafsi.

Ameongeza kuwa kufuatia kukabiliwa na chaguzi siku za usoni ni vyema Watanzania wakajiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura na kujitokeza kikamilifu katika mazoezi yote yaliyo mbele yetu kama Taifa.


END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA