USHIRIKIANO KATI YA MWAJIRI NA MTUMISHI NI CHACHU KTK MAENDELEO TAASIS- RC NDIKILO

Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/27/2015 4:46:36 PM
Imesemekana mjini Kibaha kuwa mabaraza ya wafanyakazi ni vyombo muhimu katika kuongeza ufanisi wa  kazi ikiwa pamoja na kufanya maamuzi mbalimbali yanayohusu maslahi ya wafanyakazi,taasisi na Taifa kwa ujumla.

Mkuu wa mkoa wa pwani, Mhandisi EVARIST NDIKILO ameyazungumza hayo wakati akifungua kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Rais,Tume ya mipango mjini Kibaha.

Mhandisi NDIKILO amesema ni wajibu wa mabaraza haya kama vyombo vya ushauri na usimamizi katika kuhakikisha kuwa waajiri na watumishi wanatambua wajibu na haki zao na kuzingatia maadili ya utumishi wao ili kuleta matokeo makubwa ya utendaji kazi yenye tija, staha na upendo.

Aidha mkuu huyo wa mkoa wa Pwani mhandisi NDIKILO amefafanua                kuwa hata kama kutakuwa na sera,sheria na kanuni nzuri za kazi katika eneo la kazi kama hakuna malengo ya pamoja na ushirikiano baina ya mwajiri na mwajiriwa ni vigumu taasisi hiyo kuwa na tija.

Awali akizungumza katika mkikao hicho, Kaimu Katibu mtendaji, Tume ya mipango ofisi ya Rais, BIBI.FLORENCE MWANRI amesema tume ya mipango imeshakamilisha kuandaa mwongozo wa usimamizi wa uwekezaji wa umma, ikiwa pamoja na kukamilisha tafiti mbalimbali zinazolenga katika kuharakisha maendeleo ya ukuaji wa uchumi wan chi yetu na mahitaji ya kufikia malengo ya dira ya Taifa ya maendeleo ya mwaka 2025.


END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA