Posts

Showing posts from June, 2012
Bernard Komba VURUGU ZA ZANZIBAR. Nachukizwa na baadhi ya wanasiasa na wapemba sijui waunguja kujifanya vurugu zilizotokea ni kwa minajili ya kisiasa, watu waina hiyo ndio wanaovundika mgogoro unaokuzwa na baadhi ya wanasiasa maarufu kutaka kututumbukiza katika vurugu za kidini. Watu wanaofanya vitendo hivyo wanafahaimika kwani wameanzxisha redio na magazeti kana kwamba wapo vitani wakiendesha propaganda za c...huki, lakini serikali imekuwa ikikaa kimya bila kuchukua hatua yoyote ikitegemea upole wa upande mwingine unaonyanyasika. Kwa kweli kwa mtaji ule ulioonyeshwa Visiwani na unaotaka kuonyeshwa tarehe 26, hakuna sababu yyoyote ya msingi ya kuendelea na muungano huu na tuache utabiri wa Mwalimu Nyerere utimie kwani hakuna utabiri usiotoa matokeo na alibainisha chokochoko kubwa itakuwa ni udini kutokana na serikali ya awamu ile kuiingiza Tanzania katika OIC. Hakuna kitu kitakachoweza kuzuia kuvunjika kwa muungano, vinginevyo ni matatizo kwa Tanganyika ambao wanalinganishwa na Wat

MOVEMENT 4 CHANGE YAIKUMBA PWANI.

Ben Komba/Pwani- Tanzania/Monday, June 11, 2012/17:10:32 Chama cha Demokrasia na Maendeleo Mkoa wa Pwani kimeendelea na harakati zake za kupita huko na huko kukusanya wanachjama wapya ambao ndio msingi wao katika chaguzi mbalimbali zitakazojitokeza. Katika wilaya ya Kibaha chama hicho kilifanya mkutano wa hadhara na kufanikiwa kuvuna wanachama 53 na kati yao 30 kutoka Chama Chama Mapinduzi na 23 ni wanachama huru ambao walivutika na hotuba iliyotolewa na Mbunge wa Singida mashariki, BW. TINDU LISSUambaye amewasisitiza Wana Kibaha kuamka na kuanza kuchukua hatua madhubuti kuhusiana na vuguvugu la mabadiliko ambalo limeanzishwa na CHADEMA kwa azma ya kumkomboa mwananchi wa kawaida kutoka katika kudhulumiwa. BW. LISSU amesema hali ngumu ya maisha iliyopo nchini hivi sasa sio mpango wa Mungu bali ni mpango wa Kibinadamu toka wao sio Mtume Musa bali wao ni KAISARI na kutokana na hilo mfumo huo hauna budi kubadilishwa na nguvu ya umma inahitajika katika kuelewa nia na malengo ya chama h

WASIOONA KIBAHA WAJADILI KATIBA.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/Sunday, 10 June, 2012/10:34:24 Chama cha wasioona wilaya ya Kibaha kimezungumzia suala zima la mchakato wa uandikaji wa katiba mpya ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, kwa kuhakikisha haki za watu wasioona zinaboreshwa. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mwakilishi wa wasioona Kibaha, BW. ROBERT BUNDALA amesema watu wenye ulemavu hususani wasioona wamekuwa wavumilivu kwa muda mrefu na kwa masuala mengi ya kijamii kutokana na sera na sheria mbalimbali kutoonyesha ni kwa namna gani tunastahili kuhudumiwa na kushirikishwa katika maamuzi ya mipango mbalimbali ya manedeleo ya Taifa. BW. BUNDALA ameongeza kuwa kupitia fursa hii ya mabadiliko ya katiba wanaamini kwamba ni nafasi pekee wanayotakiwa kuitumia ili kujumuisha mahitaji yetu katika katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na kufanya nchi iwe na katiba jumuishi ambayo kwa kawaida huwa ndio sheria mama ya nchi. Ameitaka serikali kujifunza kutoka nchi jirani ya Uganda na Rwanda jinsi zilivyoweka
Ben Komba/Pwani-Tanzania/12/06/09/10:33:28 Chama cha Demokrasia na Maendeleo mkoa wa Pwani, kinafanya mkutano wa hadhar wilayani Mafia katika viwanja vya Kilindoni ikiwa ni sehemu ya kujiimarisha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Kwa mujibu wa CHADEMA mkoa wa Pwani, BW. SAID UKWEZI amesema katika kuhakikisha sera za Chama chake zinafika katika kila kona ya mkoa wa Pwani, wameelekeza nguvu zao katika wilaya ambayo ni ngome ya chama cha CUF, ili kuwapatia ukombozi kupitia msemo wao wa "vua gamba vaa gwanda". BW. UKWEZI amefurahishwa na mapokezi makubwa ambayo wameyapata Kisiwani hapo yakiongozwa na Mwenyekiti wa wilaya wa chama hicho BW. ALLY MOHAMED KIGOMBA. Wakati mkutano wa hadhara wa CHADEMA unafanyika wilayani MAFIA leo, mjini Kibaha KESHO Mheshimiwa TINDU LISSU anatarajiwa kuwahutubia wananchi wa wilaya ya Kibaha vijijini hapo kesho kwenye viwanja vya stendi ya Mzenga katika utekelezaji wa kampeni yao ya MOVEMENT FOR CHANGE. Mwenyekiti wa vijana Mkoa wa Pwan

WAJUMBE WAHOJI BAJETI YA DCC INAKWENDA WAPI WILAYA YA KIBAHA?

Ben Komba/Pwani-Tanzania/6/6/2012 10:44:29 AM Mkuu wa wilaya ya Kibaha HAJAT HALIMA KIHEMBA amewahimiza wananchi kuendelea kuchangia huduma ya elimu kutokana na serikali kutokuwa na uwezo wa kufanya kila kitu kutokana na ufinyu wa bajeti uliopo. HAJAT KIHEMBA amesema hayo wakati wa kikao cha baraza la ushauri cha wilaya ya Kibaha ambapo atakaa na wakuu wa idara kuangalia jinsi gani wanaweza kuha...masisha wananchi kuhusiana umuhimu wa kuchangia huduma za elimu. Amewahimiza wazazi kuungana katika makundi ya wazazi watatu watatu ili wachangie kuweza kununua madawati kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya msingi ili kuwezesha kukabiliana na tatizo hilo. Katika hatua nyingine mmoja wa wajumbe wa kikao hicho mwakilishi wa chama cha UDP, BW. MOHAMED NGOZI ameelezea wasiwasi wake kuhusiana na maandalizi hafifu ya kikao hicho kila siku zinavyokwenda. BW. NGOZI amesema suala la Mkuu wa wilaya kuwatangazia wajumbe wa kikao kuwa hakutakuwepo na posho nah ii ikiwa mara ya pili kwa tukio kama hilo

BAJETI YA DCC KIBAHA INAENDA WAPI-Wajumbe

Ben Komba/Pwani-Tanzania/6/6/2012 10:44:29 AM Mkuu wa wilaya ya Kibaha HAJAT HALIMA KIHEMBA amewahimiza wananchi kuendelea kuchangia huduma ya elimu kutokana na serikali kutokuwa na uwezo wa kufanya kila kitu kutokana na ufinyu wa bajeti uliopo. HAJAT KIHEMBA amesema hayo wakati wa kikao cha baraza la ushauri cha wilaya ya Kibaha ambapo atakaa na wakuu wa idara kuangalia jinsi gani wanaweza kuha...masisha wananchi kuhusiana umuhimu wa kuchangia huduma za elimu. Amewahimiza wazazi kuungana katika makundi ya wazazi watatu watatu ili wachangie kuweza kununua madawati kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya msingi ili kuwezesha kukabiliana na tatizo hilo. Katika hatua nyingine mmoja wa wajumbe wa kikao hicho mwakilishi wa chama cha UDP, BW. MOHAMED NGOZI ameelezea wasiwasi wake kuhusiana na maandalizi hafifu ya kikao hicho kila siku zinavyokwenda. BW. NGOZI amesema suala la Mkuu wa wilaya kuwatangazia wajumbe wa kikao kuwa hakutakuwepo na posho nah ii ikiwa mara ya pili kwa tukio kama hilo

JENGO LA OFISI YA MKUU WA MKOA PWANI HOI

Ben Komba/Pwani-Tanzania/06:19:50 PM/18:20:00 Hali ya jengo la ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Pwani inatisha kufuatia jengo hilo kukosa miundombinu thabiti ya huduma mbalimbali kwa matumizi ya binadamu kuwa dhoofu kihali, kiasi cha kutishia mlipuko wa magonjwa ya kuambukiza au ajali mbaya.   Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia baadhi ya vyoo katika Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani ikiwa katika hali mbaya hususan wakati wa vikao vya kimkoa ambavyo vinajumuisha wajumbe kutoka wilaya mbalimbali za mkoa wa Pwani ambavyo vinahudhuriwa na wajumbe wengi, vyoo vinakuwa havitamaniki.   Mmoja wa watu nilioongea nao amesema vyoo hivyo vinatofauti kidogo tu na vyoo vya umma ambavyo havina uangalizi wowote, na mbali ya tatizo hilo la vyoo katika jengo hilo kuwa ni suala la kupigiwa chapuo, na wakati mwingine maji kutoka chooni kutitirika mpaka maofisini na kusababisha sehemu ya jengo hilo kuwa wazi kutokana na tatizo hilo.   Kwa upande wa mbele wa jengo hilo kulipo milango miwili mikubwa ya mba

TATHM9INI YA ELIMU YA UWEZO-TWAWEZA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/6/6/2012 11:17:24 AM Mafunzo maalum kwa watafiti wa kujitolea ambao wanapatiwa mafunzo maalum kwa ajili ya kwenda kufanya tathmini kwa kutumia dodoso maalum ili kujua ushiriki wa wanafunzi katika masomo, Kiingereza, hisabati, kiswahili na kusoma. Mwezeshaji kutoka PWANI-DPA, BW. MATTHEW CHUNGU amesema malengo ni kuwajengea uwezo watafiti wasaidizi kupitia mradi wa UWEZO- ...TWAWEZA ambapo mradi huo pia unatekelezwa katika nchi za UGANDA na KENYA. BW. CHUNGU amebainisha kuwa matokeo ya utafiti utakaofanywa utasaidia kuipa taarifa jamii kuhusiana na maendeleo ya elimu nchini, ili kuweka mikakati ya pamoja katika kuboresha kiwango cha elimu nchini. BW.CHUNGU ameongeza kuwa mbinu itakayotumika kuwapima ni pamoja na kuchukua vijana wa miaka 6-16 na kuwatathmini kupitia kitabu cha darasa la pili ili kujua uwezo wao wa kuelewa. Ameongeza Mpango huo wa miaka mitatu unatarajiwa kufikia vijiji 30 na katika kila kijiji wanategemea kufikia kaya 20, na matarajio yao ni j