WAJUMBE WAHOJI BAJETI YA DCC INAKWENDA WAPI WILAYA YA KIBAHA?
Ben Komba/Pwani-Tanzania/6/6/2012 10:44:29 AM
Mkuu wa wilaya ya Kibaha HAJAT HALIMA KIHEMBA amewahimiza wananchi kuendelea kuchangia huduma ya elimu kutokana na serikali kutokuwa na uwezo wa kufanya kila kitu kutokana na ufinyu wa bajeti uliopo.
HAJAT KIHEMBA amesema hayo wakati wa kikao cha baraza la ushauri cha wilaya ya Kibaha ambapo atakaa na wakuu wa idara kuangalia jinsi gani wanaweza kuha...masisha wananchi kuhusiana umuhimu wa kuchangia huduma za elimu.
Amewahimiza wazazi kuungana katika makundi ya wazazi watatu watatu ili wachangie kuweza kununua madawati kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya msingi ili kuwezesha kukabiliana na tatizo hilo.
Katika hatua nyingine mmoja wa wajumbe wa kikao hicho mwakilishi wa chama cha UDP, BW. MOHAMED NGOZI ameelezea wasiwasi wake kuhusiana na maandalizi hafifu ya kikao hicho kila siku zinavyokwenda.
BW. NGOZI amesema suala la Mkuu wa wilaya kuwatangazia wajumbe wa kikao kuwa hakutakuwepo na posho nah ii ikiwa mara ya pili kwa tukio kama hilo kujitokeza na mbaya zaidi katika kikao hiki hata chakula kwa wajumbe kilipatikana kwa tabu na baadhi ya wajumbe kukosa kabisa.
BW. NGOZI ameitaka mamlaka husika kuliangalia kwa undani suala hilo kwani linaonekana kuwa desturi, kwani kikao hicho kipo kisheria na moja ya kikao kinachotumia fedha nyingi katika halmashauri na matokeo yake fedha haziwafikii walengwa.
Kikao cha baraza la ushauri cha wilaya wajumbe wake ni pamoja na viongozi wa dini, watendaji wa halmashauri, viongozi wa vyama vya siasa na wadau wengine.
END
Comments
Post a Comment