MOVEMENT 4 CHANGE YAIKUMBA PWANI.
Ben Komba/Pwani- Tanzania/Monday, June 11, 2012/17:10:32
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Mkoa wa Pwani kimeendelea na harakati zake za kupita huko na huko kukusanya wanachjama wapya ambao ndio msingi wao katika chaguzi mbalimbali zitakazojitokeza.
Katika wilaya ya Kibaha chama hicho kilifanya mkutano wa hadhara na kufanikiwa kuvuna wanachama 53 na kati yao 30 kutoka Chama Chama Mapinduzi na 23 ni wanachama huru ambao walivutika na hotuba iliyotolewa na Mbunge wa Singida mashariki, BW. TINDU LISSUambaye amewasisitiza Wana Kibaha kuamka na kuanza kuchukua hatua madhubuti kuhusiana na vuguvugu la mabadiliko ambalo limeanzishwa na CHADEMA kwa azma ya kumkomboa mwananchi wa kawaida kutoka katika kudhulumiwa.
BW. LISSU amesema hali ngumu ya maisha iliyopo nchini hivi sasa sio mpango wa Mungu bali ni mpango wa Kibinadamu toka wao sio Mtume Musa bali wao ni KAISARI na kutokana na hilo mfumo huo hauna budi kubadilishwa na nguvu ya umma inahitajika katika kuelewa nia na malengo ya chama hicho.
Akizungumzia kuhusu muungano BW. LISSU amesema suala hilo kimsingi halina maana kwa mwananchi wa kawaida badala yake umekuwa ni muungano wa kugawana vyeo tu na sio wananchi wa nchi mbili hizi toka Zanzibar imeamua kuwa na katiba yake yenyewe, wimbo wa Taifa wake, Amiri Jeshi wake mkuu, majeshi na hata mahakama sasa nchi moja itrakuwaje na katiba mbili.
Amesisitiza hakuna ajabu yoyote kwa Tanganyika kutengana, toka katika karne hii kuna nchi nyingi zilizokuwa muungano zimetengana akitoa mfano wa nchi za Eritrea na Ethiopia CZECH na SLOVAKIA na Jamhuri ya Kisoviet na YUGOSLAVIA ambayo imetoa mataifa ya Bosnia, Croatia, Macedonia na Serbia, hivyo wakati ukifika sio vibaya tukatengana na hilo lisifanywe jambo lisiloepukika.
Wakati Kibaha yakijiri hayo huko wilayani Mafia Kisiwani chama cha CHADEMA kimefanikiwa kupata wanachama wa 450 wapya kutokana kampeni ya vuguvug la mabadiliko ambalo chama hicho kinajipanga kuchukua dola itakapofika mwaka 2015.
Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Pwani, BW. SAID UKWEZI amesema wanachama hao wamewapata kufuatia kufanya mikutanoya hadhara katika maeneo ya Kilindoni na Kilongwe, ambapo kati ya haowanachama kutoka CCM ni 50, CUF 70 nnna wanachama wa kawaida ni 100 hao ni wale waliojiunga katika mkutano wa Kilindoni.
Na katika mkutano uliofanyika katika kata ya Kilongwe wanachama 200 walijiunga na chama hicho kati yao TLP 18, CUF 20, CCM 11 na 51 ni wanachama huru.
Nako wilayani Kisarawe Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kimefanikiwa kunyakua uongozi mzima wa kijiji cha Mwanzo Mgumu katika uchaguzi wa marudio kufuatia ule wa awali kuvurugika kufuatria baadhi ya watu wasiojulikana kuiba masanduku ya kura na kutokomea kusikojulikana.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Chama hicho amesema katika kijiji hicho wamefanikiwa kumpata Mwenyekiti wa kijiji, BW. SAID ATHUMAN MLUGENDO na wajumbe wote wa halmashauri ya kijiji.
END.
Comments
Post a Comment