TATHM9INI YA ELIMU YA UWEZO-TWAWEZA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/6/6/2012 11:17:24 AM Mafunzo maalum kwa watafiti wa kujitolea ambao wanapatiwa mafunzo maalum kwa ajili ya kwenda kufanya tathmini kwa kutumia dodoso maalum ili kujua ushiriki wa wanafunzi katika masomo, Kiingereza, hisabati, kiswahili na kusoma. Mwezeshaji kutoka PWANI-DPA, BW. MATTHEW CHUNGU amesema malengo ni kuwajengea uwezo watafiti wasaidizi kupitia mradi wa UWEZO- ...TWAWEZA ambapo mradi huo pia unatekelezwa katika nchi za UGANDA na KENYA. BW. CHUNGU amebainisha kuwa matokeo ya utafiti utakaofanywa utasaidia kuipa taarifa jamii kuhusiana na maendeleo ya elimu nchini, ili kuweka mikakati ya pamoja katika kuboresha kiwango cha elimu nchini. BW.CHUNGU ameongeza kuwa mbinu itakayotumika kuwapima ni pamoja na kuchukua vijana wa miaka 6-16 na kuwatathmini kupitia kitabu cha darasa la pili ili kujua uwezo wao wa kuelewa. Ameongeza Mpango huo wa miaka mitatu unatarajiwa kufikia vijiji 30 na katika kila kijiji wanategemea kufikia kaya 20, na matarajio yao ni jamii iweze kutumia matokeo kwa kuibua mjadala na kukabiliana na changamoto zilizopo katika sekta ya elimu. BW. CHUNGU akibainisha mafanikio ambayo yamepatikana mpaka sasa ni serikali kutambua jitihada zao katika suala zima la kunyanyua kiwango cha elimu na kuleta uwiano wa kielimu katika nchi za Afrika Mashariki. END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA