JENGO LA OFISI YA MKUU WA MKOA PWANI HOI
Ben Komba/Pwani-Tanzania/06:19:50 PM/18:20:00
Hali ya jengo la ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Pwani inatisha kufuatia jengo hilo kukosa miundombinu thabiti ya huduma mbalimbali kwa matumizi ya binadamu kuwa dhoofu kihali, kiasi cha kutishia mlipuko wa magonjwa ya kuambukiza au ajali mbaya.
Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia baadhi ya vyoo katika Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani ikiwa katika hali mbaya hususan wakati wa vikao vya kimkoa ambavyo vinajumuisha wajumbe kutoka wilaya mbalimbali za mkoa wa Pwani ambavyo vinahudhuriwa na wajumbe wengi, vyoo vinakuwa havitamaniki.
Mmoja wa watu nilioongea nao amesema vyoo hivyo vinatofauti kidogo tu na vyoo vya umma ambavyo havina uangalizi wowote, na mbali ya tatizo hilo la vyoo katika jengo hilo kuwa ni suala la kupigiwa chapuo, na wakati mwingine maji kutoka chooni kutitirika mpaka maofisini na kusababisha sehemu ya jengo hilo kuwa wazi kutokana na tatizo hilo.
Kwa upande wa mbele wa jengo hilo kulipo milango miwili mikubwa ya mbao, mpaka sasa mlango mmoja unalazimika kulala bila kufungwa kutokana na bawaba za mlango kuharibika na hivyo kutishia maisha ya kila mmoja anayeingia katika jengo hilo kupitia mlango huo mkubwa kwani mlango huo unaweza kuanguka wakati wowote, kiasi cha kulifanya jengo hilo kama halina mwenyewe.
Mmoja wa wadau wa kijamii niliyeoongea naye BW. HUSSEIN HUSSEIN amesikitishwa na hatua ya wahusika ambao anaamini wapo ndani ya jengo hilohilo klufumbia macho hali hiyo ikiwa pamoja na sehemu ya nyuma ya jengo hilo kuwa chafu kiasi cha kutia aibu.
Katika kikao cha ushauri cha mkoa wa Pwani kilichofanyika mjini Kibaha katika taarifa ambayo imesomwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, BI. BEATHA MMARI imebainisha kuwa katika kipindi cha robo ya mwaka wa fedha 2011/2012 ofisi ya mkuu wa mkoa wa Pwani ilitarajia kutekeleza miradi ya ukarabati wa ofisi ya mkuu wa mkoa, ukarabati wa jengo la mkuu wa wilaya ya Kibaha ikiwa ni awamu ya pili, ujenzi wa nyumba ya katibu tawala wilaya ya Mafia awamu ya 3 ambapo miradi hiyo yote haijatekelezwa kwa kile kinachodaiwa fedha ambazo zimepatikana zilielekezwa kulipa madeni ya nyuma.
END
Comments
Post a Comment