Posts

Showing posts from February, 2013

RAGE AFUNGUA TAWI SIMBVA TISHIO KIBAHA.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/25-Feb-13/18:50:15 Mwenyekiti wa klabu ya Simba maarufu kama wekundu wa Msimbazi amezindua rasmi tawi namba 11 la SIMBA TISHIO lillilopo Katika Mtaa wa Kwa mfipa mjini Kibaha na kuongea na wanachama na washabiki wa timu hiyo mjini Kibaha. Akizungumza katika mkutano huo amewataka wana simba kutoachia klabu hiyo watu wasio na uwezo wa kifedha kutokana na mpira kwa hivi sasa kutawaliwa na fedha, amebainisha uwepo wa gharama mbalimbali ambazo wakati mwingine inakuwa haina uwezo wa kifedha kuzilipa na kama kiongozi unahitajika wakati wote kuwa na jibu muafaka kuhusiana na kila kinachotokea klabuni. Mwenyekiti RAGE amesikitishwa na baadhi ya magazeti ya Michezo kwa kupotosha taarifa mbalimbali kwa lengo la kutaka kuuza magazeti na kuwachanganya wapenzi na washabiki wa soka, akitoa mfano habaria ambayo gazeti moja la michezo nchini lilitoa ya kuwa Malkia wa Nyuki hawahitaji RAGE na KABURU kitu ambacho sio kweli Kabisa. Naye Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM am

OPERESHENI SENSA 2012.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/21 February, 2013/15:59:31 Kikosi namba 832 cha Jeshi la kujenga Taifa Ruvu, kimetoa wahitimu 994 wa mafunzo ya awali ya kijeshi ya vijana maarufu kama operesheni sensa 2012 ikiwa ni mhafali ya 102 tangu kuanzishwa kwa Jeshi hilo ambapo kati ya wahitimu hao wavulana ni 754 na wasichana 240. Kwa mujibu wa risala iliyosomwa na mmoja wa wahitimu hao AFANDE. MARTIN MABENA, inasema kuna baadhi ya hao vijana walioshiriki mafunzo hayo ya opersheni sensa kuna walioshindwa kuhitimu mafunzo hayo kutokana na sababu za kiafya ni mmoja, vifo wawili, utovu wa nidhamu wawili na kuwa na jumla ya wahitimu watano walioshindwa kuhitimu mafunzo hayo kati yao wavulana wakiwa wawili na wasichana watatu. AFANDE MABENA amesema katika risala hiyo kuwa malengo ya operesheni sensa ni kujenga uzalendo na uvumilivu miongoni mwa vijana wa Tanzania, ikiwa pamoja na kuwaanda kuwa raia wema ili kuwezesha upatikanaji wa viongozi bora watakaoweza kuiilinda nchi na kuitumikia kwa malengo

MAJI CHANZO KIBAHA WANAOFAIDIKA NI WA DAR ES SAALAM.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/16-Feb-13/20:23:45 Kukosekana kwa maji ya bomba kwa takriban mwezi mmoja kumesababisha Diwani wa Kata ya Mailimoja mjini Kibaha BW. ANDREW LUGANO kufanya ziara ya ghafla katika ofisi ya DAWASCO katika mkoa wa Pwani kutaka kujua ni nini chanzo cha ukosefu wa maji katika mji huo ili hali chanzo kipo mkoani mwao. Katika Ofisi za DAWSCO tulibahatika kumkuta Meneja wa DAWASCO, BW. ROBERT MUGABE ambaye baada ya kuelezwa kuhusu tatizo hilo ukapita uamuzi wa meneja huyo ambaye alidai maji jana yake yalitoka kuambatana na diwani huyo kwenda kumuonyesha maeneo ambayo maji kwao sasa ni kitendawili. Baadhi ya maeneo ambayo yalifikiwa na Meneja huyo wa DAWASCO kushuhudia mwenyewe kutokuwepo maji na uhariobifun wa miundo mbinu ambayo DAWASCO wamezembea kufanya ukarabati na wakijua kutofanya hivyo ni kusababisha wateja kukosa huduma hiyo muhimu kwa binadamu. Baadhi ya wananchi wameelezea kukerwa kwao na wasoma mita ambao wamekuwa wakifika majumbani kwao ilihali wakij

FULL COUNCIL TC

Ben Komba/Pwani-Tanzania/21-Feb-13/18:38:58 Katika utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2012/2013 halmashauri ya mji wa Kibaha imefanikiwa kutekeleza na kuimarisha utoaji wa huduma katika kwa ufanisi mkubwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo afya,usafi wa mazingira, elimu na uimarishaji wa miundo mbinu ya barabara ikiwa pamoja na kununua greda. Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Kibaha, BI.JENIFA OMOLO amebainisha kuwa halamshauri yake katika kipindi cha fedha kinachoishia Julai mwaka huu, ilikadiria kukusanya shilingi bilioni 18 lakini mpaka sasa kiasi kilichokusanywa ni shilingi bilioni nane tu, na juhudi zinafanyika katika kuhakikisha lengo hilo linafikiwa au kuvukwa kwa kubuni vyanzo mbalimbali vya kujikusanyia mapato. BI.OMOLO ameongeza kuwa halmashauri yake imelenga kukusanya mapato hayo katika vyanzo mbalimbali ikiwemomaegesho ya magari, machimbo ya mchanga, kodi za majengo, kodi ya ardhi na msurur wa kodi nyingine mbalimbali kama ilivyoainishwa katika hotuba ya bajeti

DailyNews Mobile Edition - State condemns priest’s murder

DailyNews Mobile Edition - State condemns priest’s murder

MKURUGENZI SHIRIKA ASHUTUMIWA

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/15-Feb-13/18:54:49 Kufuatia kupatikana kwa vipeperushi vinavyosemekana vimechapishwa na wafanyakazi wa shirika la elimu Kibaha zenye kushutumu uongozi wa shirika hilo chini ya Mkurugenzi mtendaji BW. CYPRIAN MPEMBA kwa kupendelea baadhi ya wafanyakazi na kuwaweka wengine pembeni. Kipeperushi hicho kilichomfikia mwandishi wa habari hizi kikiwa na malalamiko kadhaa yanayomshutumu Mkurugenzi wa Shirika la elimu Kibaha kuhusiana na masuala mbalimbali likiwamo kumtaka amuondoe Afisa Tawala wake na kudai kwamba ni mtu anayemshauri juu ya ubaya wa wengine ilihali akificha ya kwake. Mbali ya lawama hizo kipeperushi hicho kilifika mbali kwa kudai mkurugenzi huyo amekuwa akikataa kutoa fursa kwa wafanyakazi kwenda kujisomea kwa madai ya kuwa shirika halina fedha na wakati huohuo anatoa nafasi kwa mfanyakazi mmoja kwenda kusomea PHD kutokana tu na ukaribu wao. Akijibu tuhuma hizo Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la elimu Kibaha, DKT. CYPRIAN MPEMBA amesema anachoja

Members of Congress Demand Obama Administration Classify Ft. Hood Attack an 'Act of Terrorism' - ABC News

Members of Congress Demand Obama Administration Classify Ft. Hood Attack an 'Act of Terrorism' - ABC News

TADERE NA MPANGO MKAKATI.

Image
Ben Komba/Pwani-Tanzania/13/02/13/03:39:49 PM Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na ufanyaji wa utafiti kuhusu watu wenye ulemavu wa kusikia, linatengeneza mpango kazi maalum wa kipindi cha miaka mitatu katika kuhakikisha wanafuata kanuni na utaratibu mzima wa uendeshaji asasi za kiraia. Akizungumza katika zoezi hilomwezeshaji, BW. ISRAEL ILUNDE amesema lengo la mpango kazi ni kuweka makubaliano ya awali juu ya mwelekeo na mchakato mzima wa maandalizi ya mpango mkakati wa utekelezaji wa asasi katika kipindi cha miaka mitatu. BW. ILUNDE amebainisha kuwab vitu ambavyo ni muhimu kuju;likana mapema ni madhumuni na hatua zitakazopitiwa, muda wa kuanza na kukamilisha kusudio lao, kwa kuweka jukumu, wajibu wa asasi kwa kuzingatia katiba ya asasi na nyaraka zingine za kisheria au taarifa ya utekelezaji ya mpango mkakati uliuopita. Naye Mkurugenzi wa asasi ya TADERE, BW. NIDROSSY MLAWA, kutokana na kundi hilo kukabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zilikuwa hazijawahi

WADAU WA ELIMU.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/12 February, 2013/14:40:45 Masuala ya ruzuku na kukosekana kwa walimu wa kike wa kutosha katika maeneo ya pembezoni kumezua mjadala wa kadiri katika kikao cha wadau wa elimu katika halmashauri ya wilaya Kibaha, chenye lengo la kung'amua mafanikio na mapungufu katika suala zima la usimamizi wa elimu. Mmoja wa wajumbe waliohudhuria kikao hicho kutoka katika Kata ya Magindu amelalamikia idara ya elimu kwa kuzorotesha upelekaji wa ruzuku ya dola kumi kwa kila mwanafunzi na hivyo kuathiri uboreshaji wa elimu, amefafanua upatikanji wa fedha hizo umekuwa na mizengwe mingi na hata zikipatkana zinakuwa zimeshachelewa. Mjumbe huyo ameitaka serikali kuhakikisha inafikisha fedha za ruzuku kwa wakati na wachukulie suala hilo kama wajibu na sio hisani kama watendaji wengi wanavyolichukulia na kusaidia kuwaepusha baadhi ya watendaji kujikuta wanatoa fedha za mifukoni mwao kuendesha shughuli za shule. Naye Mwenyekiti wa Kamati ya shule ya msingi MUYUMBO, BW. MORETO

M4C NA POLICE WAAGANA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/10-Feb-13/13:42:54 Chama cha demokrasia na maendeleo kimewataka wananchi kutokubali kurubuniwa kwa kuwaambia CHADEMA ni chama cha kidini kunakosababishwa kwa baadhi ya vyama kutumia propaganda hiyo kutaka kuwagawa watanzania na baadaye kuwatawala kwa kufuata mifumo ya kurithishana kama inavyojidhihirisha hivi sasa. Akiongea katika mkutano wa vuguvugu la mabadiliko inayoendelea nchi hivi sasakatika viwanja vya stendi ya Mzenga katika mamlaka ya mji mdogo wa Mlandizi yenye kulenga kutekeleza kauli ya mwaka wa nguvu ya umma inayoeendeshwa na chama cha demokrasia na kufanikiwa kuleta mitazamo chanya kwa wakazi wa wilaya ya Kibaha kutokana na kuwepo piga nikupige ya mikutano kati ya chama cha CHADEMA na CCM. Kada wa chama cha demokrasia na maendeleo kutoka Arusha, BW.ALLY BANANGA amesema cha cha CCM kimekuwa chama cha kurithisha uongozi na kuyatupa kando malengo ya awali ya uanzishaji wa chama hicho ambayo yalikuwa hayana lengo la kujenga himaya za kisultani
Ben Komba/Pwani-Tanzania/10-Feb-13/13:42:54 Chama cha demokrasia na maendeleo kimewataka wananchi kutokubali kurubuniwa kwa kuwaambia CHADEMA ni chama cha kidini kunakosababishwa kwa baadhi ya vyama kutumia propaganda hiyo kutaka kuwagawa watanzania na baadaye kuwatawala kwa kufuata mifumo ya kurithishana kama inavyojidhihirisha hivi sasa. Akiongea katika mkutano wa vuguvugu la mabadiliko inayoendelea nchi hivi sasakatika viwanja vya stendi ya Mzenga katika mamlaka ya mji mdogo wa Mlandizi yenye kulenga kutekeleza kauli ya mwaka wa nguvu ya umma inayoeendeshwa na chama cha demokrasia na kufanikiwa kuleta mitazamo chanya kwa wakazi wa wilaya ya Kibaha kutokana na kuwepo piga nikupige ya mikutano kati ya chama cha CHADEMA na CCM. Kada wa chama cha demokrasia na maendeleo kutoka Arusha, BW.ALLY BANANGA amesema cha cha CCM kimekuwa chama cha kurithisha uongozi na kuyatupa kando malengo ya awali ya uanzishaji wa chama hicho ambayo yalikuwa hayana lengo la kujenga himaya za kisultani

TANZANIA COALITION ON DEBT AND DEVELOPMENT.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/13/02/11/17:40:47 Mtandao unaojishughulisha na madeni na maendeleo nchini umepongeza wilaya ya Kibaha kwa kuweza kuwashawishi watoto wa wa kike kujiendeleza kielimu ikiwa pamoja na kuwepo na ahueni katika uwiano unaoridhisha kati ya walimu na wanafunzi ambapo kwa sasa mwalimu mmoja anafundisha watoto 35 kulinganisha na maeneo mengine Mkurugenzi wa mtandao wa madeni na maendeleo nchini, BW. HEBRON MWAKAGENDA ametoa pongezi hizo kwa halmashauri zote mbili za wilaya ya Kibaha wakati wa kuwasilisha ripoti ya utafiti kuhusiana na hali ya elimu na afya kwa wilaya kadhaa nchini, kwa kuweza angalau kukabiliana na mapungufu mbalimbali ikiwa pamoja na kuweka mazingira mazuri ya utoaji na upatakanaji wa huduma ya elimu. BW. MWAKAGENDA amebainisha kuwa sekta ya elimu ni ni moja ya vipaumbele muhimu katia utekelezaji wa mpango mzima wa MKUKUTA ikiwa ni nguzo mojawapo ya kuboresha maisha ya jamii kwa ujumla, utafiti wao wameufanya katika wilaya saba za Morogoro, Kiba

NHIF - PWANI

NHIF PWANI Ben Komba/Pwani-Tanzania/08-Feb-13/8:09:28 Mfuko wa Bima ya afya katika mkoa wa Pwani umewataka wadau wa mfuko huo kufanya kazi za utoaji huduma za mfuko huo kwa kushirikiana na kutimiza wajibu kwa kila mtu na eneo lake ili kukabiliana na chnagamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika uendeshaji wa mfuko huo. Meneja wa mfuko wa Bima ya afya katika mkoa wa Pwani, BW. ANDREW MWILUNGU amesema kuwa ofisi ya mkoa wa Pwani imezinduliwa rasmi Oktoba 3, 2002 na toka kuanzishwa kwake wamekuwa wakifanya kazi karibu na waandishi katika kuhakikisha wananchi wanapata taarifa za kutosha kuhusiana na mfuko huo. BW. MWILUNGU amebainisha kuwa ufanisi katika mkoa wa Pwani umeongezeka kutokana na sasa kuwepo na usimamizi wa karibu wa utekelezaji wa malengo ya mfuko huo kwa kusimamia kwa karibu wadau wengine ambao wanahusika katika zoezi zima la kutoa huduma kupitia mfuko huo. Meneja huyo wa Mfuko wa Bima ya afya katika mkoa wa Pwani, BW. ANDREW MWILUNGU amebainisha kuwa kwa sasa w

LAW DAY

Ben Komba/Pwani-Tanzania/06-Feb-13/15:21:57 Wananchi na watendaji wametakiwa kuheshimu sheria bila kushurutishwa, ili kuweza kujenga utawala ambao utafuata misingi ya sheria bila upendeleo wala ubaguzi wowote ili kuweza kudumisha amani na utulivu uliopo nchini. Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya sheria katika mkoa wa Pwani, Hakimu mkazi mwandamizi mfawidhi wa mkoa wa Pwani, Mheshimiwa BAHATI NDESERUA amesema katika ujenzi wa utwala wa sheria ambao utazingatia haki ya kila mmoja bila kujali itikadi au uwezo wa mtu binafsi, kwani hakuna mtu ambaye yupo juu ya sheria kama Mwanafalsafa SOCRATES aliyewahi kusema "Mfalme hawezi kuwa chini ya mtu, bali ni chini ya Mungu na sheria". Hakimu Mkazi mfawidhi mwandamizi, BI.NDESERUA ameongeza katika kuitafakari siku hii ni vyema kutambua utawala wa sheria ni bora kuliko uhuru binafsi, na maana halisi ya utawala wa sheria kila mmoja wetu anapaswa kutendewa haki bila kujali uwezo au itikadi, kwani mbele ya sheria sisi sote ni

Wanted Arsal man had links to Al-Qaeda: Lebanese Army

Wanted Arsal man had links to Al-Qaeda: Lebanese Army

Egypt pope criticizes constitution

Egypt pope criticizes constitution

Natural Cures Not Medicine: Garlic Oil Kills cancer

Natural Cures Not Medicine: Garlic Oil Kills cancer

Natural Cures Not Medicine: Cancer Cure Hemp Oil - Rick Simpson and testimonies

Natural Cures Not Medicine: Cancer Cure Hemp Oil - Rick Simpson and testimonies

KAMPENI YA MAMA MISITU RUVU KUSINI.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/05-Feb-13/02:47:28 PM Mpango wa Mama misitu wenye lengo la kuhifadhi misitu ya asili katika msitu wa Ruvu kusini katika wilaya za Kibaha na Kisarawe, umeingia awamu ya pili ambayo italenga katika kuwajengea uwezo viongozi katika ngazi mbalimbali kuweza kulinda na kuisimamia misitu kwa umakini. Mratibu wa Mama Misitu katika msitu wa Ruvu kusini, BW. YAHYA MTONDA amesema kwa upande wa wananchi mpango huo umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani wakazi wa vijiji kumi vya majaribio wananchi wamepata mwamko wa kutosha kuhusiana na utunzaji wa misitu katika eneo hilo la Ruvu Kusini. BW. MTONDA amebainisha kwa sasa wanatgegemea kuwafikia viongozi wa kata na wilaya ili kuwapatia elimu zaidi juu ya umuhimu wa kulinda misitu ya asili kama ilivyofanyika kwa wananchi ambao kwa sasa wenyewe wamefikia hatua ya kufanya doria katika msitu wa Ruvu kusini, ikiwa pamoja na kutoa taarifa wanapoona uharibifu wowote unafanyika. Amesema kampeni ya mama msitu kampeni inafanya ka

UWT KATA YA TUMBI YATOA MSAADA HOSPITALI YA TUMBI.

UWT KTA YA TUMBI YATOA MSAADA KWA WAGONJWA. Ben Komba/Pwani-Tanzania/02-Feb-13/17:38:00 Jumuiya ya wanwake wa chama cha mapinduzi wametembelea hospitali Maalum ya rufaa ya Tumbi iliyopo mjini Kibaha katika mkoa wa Pwani, ambapo walitumia fursa hiyo kutoa msaada wa kiutu kwa wagonjwa ambao wamelazwa katika wodi ya watoto na kufanya usafi kuzunguka maeneo ya hospitali. Mwenyekit wa jumuiya ya wanawake kata ya Tumbi, BIBI. CLEMENTINA NGONYANI amesema tukio hilo nim maadhimisho a miaka 36 ya kuzaliwa kwa chama hicho, ambapo kilele chake ni siku ya Jumapili Februari kimkoa na maadhimisho yake yatafanyika Utete wilayani Rufiji ambapo wageni mbali mbali wameshaelekea huko. BIBI. NGONYANI amebainisha kwa kufanya hivyo kutasidia kukiweka chama hicho karibu na wananchi na kuweza kuwaelekeza kuwa CCM ndio chama imara ambacho kitaweza kuwakomboa wananchi kutoka katika hali duni mpaka kufikia matarajio yao wakipea nafasi zaidi. Katibu wa Jumuiya ya wanawake katika Kata ya Tumbi, BIBI GE

MAHABUSU WAPATA BASI LA

MAHABUSU WAPATA BASI LA KUWABEBA PWANI. Ben Komba/Pwani-Tanzania/01-Feb-13/8:47:00 Jukumu la kusafirisha mahabusu kutoka wanakoshikiliwa kupelekwa mahakamani mjini Kibaha limekabidhiwa rasmi kwa Jeshi la magereza katika suala zima la kuleta mabadiliko ya kiutendaji katika idara mbili hizo za serikali. Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia Basi la kubeba Mahabusu likiwa eneo la mahakama ya Mkoa wa Pwani, kufuatia uzinduzi uliofanyika katika gereza la Ubena na kuzinduliwa rasmi na Naibu waziri wa Mambo ya ndani, BW. PERREIRA AME SILIMA na kushuhudia na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa. Mkoa wa Pwani ni mmoja wa wa mikoa ambayo imezindua utaratibu huo ambao kwa sasa utahakikisha usalama wa mahabusu na askari kutokana na kupata basi hilo maalum kwa ajili ya kazi ya kubeba mahabusu, tofauti na awali ambapo walikuwa wakipakizwa katika LAND ROVER na kufanya askari kulazimika kuning'inia huku akiwa ameshika bunduki, hali ambayo ilisababisha baadhiu ya wafungwa kutoroka. Baad