TADERE NA MPANGO MKAKATI.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/13/02/13/03:39:49 PM
Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na ufanyaji wa utafiti kuhusu watu wenye ulemavu wa kusikia, linatengeneza mpango kazi maalum wa kipindi cha miaka mitatu katika kuhakikisha wanafuata kanuni na utaratibu mzima wa uendeshaji asasi za kiraia.
Akizungumza katika zoezi hilomwezeshaji, BW. ISRAEL ILUNDE amesema lengo la mpango kazi ni kuweka makubaliano ya awali juu ya mwelekeo na mchakato mzima wa maandalizi ya mpango mkakati wa utekelezaji wa asasi katika kipindi cha miaka mitatu.
BW. ILUNDE amebainisha kuwab vitu ambavyo ni muhimu kuju;likana mapema ni madhumuni na hatua zitakazopitiwa, muda wa kuanza na kukamilisha kusudio lao, kwa kuweka jukumu, wajibu wa asasi kwa kuzingatia katiba ya asasi na nyaraka zingine za kisheria au taarifa ya utekelezaji ya mpango mkakati uliuopita.
Naye Mkurugenzi wa asasi ya TADERE, BW. NIDROSSY MLAWA, kutokana na kundi hilo kukabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zilikuwa hazijawahi kufanyiwa utafiti wa kina, walianzisha asasi hiyo kwa lengo la kubaini na kuanika changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wenye ulemavu wa kusikia.
BW. MALAWA ameongeza taasisi yao imehakikisha katika kuhakikisha mpango mkakati wao wa kipindi cha miaka mitatu ijayo unakuwa na tija na mafanikio wamechukua fursa hiyo kushirikisha watu kutoka katika makundi mbalimbali ya kijamii, taasisi binafsi na za umma ili kwa pamoja waweze kupanga mpango ambao utasaidia kutosahauliwza kwa kundi hilo katika masuala mbalimbali ya kitaifa.
BW.NIDROSY MLAWA mkurugenzi wa TADERE amefafanua kuwa kwa upande wa watu wenye ulemavu wa kusikia wanapata wakati mgumu katika masuala mbalimbali ya kitaifa kama mchakato wa kutafuta katiba mpya na sasa vitambulisho vya uraia, ambapo wakati mwingine ukiuliza hata ambao hawana ulemavu wanakwambia na wenyewe hawaelewi vizuri.
Nilibahatika kuongea na Mwalimu ANNA LULANDALA, anayefundisha watoto wenye ulemavu wa kusikia katika moja ya shule za msingi Mlandizi ambaye yeye meelezea changamoto ya kukosekana vifaa maalum vya kufundishia watoto hao imekuwa kikwazo kikubwa katika kuwapatia elimu ya kiwango stahili wanafunzi hao wenye ulemavu wa kusikia.
END.
Comments
Post a Comment