MAMLAK YA MJI MDOGO MLANDIZI HOI.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/
Wananchi katika mamlaka ya mji mdogo wa Mlandizi wamelalamika hatua ya uanzishaji wa mji huo na kuutelekeza bila kuiwezesha kifedha hali inayoathiri utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya kila siku.
Nikiongea na mmoja wa wajumbe wa baraza la mamlaka ya mji mdogo wa Mlandizi ambaye alikataa jina lake kutajwa , amebaiinisha kuwa kumekuwepo na changamoto mbalimbali zinazoikabili mamlaka ya mji mdogo wa Mlandizi.
Mjumbe huyo amesema kutokana na kukosekana kwa fedha kutoka halmashauri kunakosabishwa na baadhi ya watendaji ya halmashauri kuchelea wao kupunguza fedha za uendeshaji wa halmashauri kutokana na kutojiamini.
Mjube huyo amebainisha kutokuwepo kwa vikao vya kisheria vya kila mwaka vinavyofanywa na baraza la mamlaka ya mji mdogo wa Mlandizi kwa madai ya kukosekana kwa fedha na kuhoji serikali inawezaje kupanga mipango ambayo haiwezi kuitekeleza.
Naye Mwenyekiti wa mamalaka ya mji mdogo wa Mlandizi, BW. ABDALLAH KIDO amesema ni kweli wamekuwa wakipata wakati mgumu kutokana na ukosefu wa fedha na hivyo kufanya utendaji wa mamlaka ya mji mdogo kuzorota.
BW. KIDO amesema mamlaka ya mji mdogo wa Mlandizi inakusanya takriban asilimia 75 ya mapato jumla ya halamashauri na fedha hizo kutrudishwa kwa ajili ya uendeshaji wa Baraza la mji mdogo wa Mlandizi ambalo lina majukumu ya kupanga, kuratibu na kusimamia maendeleo ya mji mdogo wa Mlandizi.
END.
Comments
Post a Comment