AKAMATWA AKIWANGA.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/26-May-13/19:36:49 Kijana mmoja anayejulikana kwa jina moja tu la UBAYA amenusurika kuuwawa kufuatia kukutwa ndani ya chumba ambacho kilikuwa kimefungwa milango na madirisha kwa umakini mkubwa bila mafanikio. Akielezea mkasa huo Mama ISMAIL ambaye mtoto wake ISMAIL mwenye umri wa miaka mitatu alikuwa ndio lengo la mtu huyo anayesadikiwa kuwa ni mshirikina kutokana na maelezo ambayo aliyatoa mara baada ya kumwagiwa maji ya baraka. Katika kumdadisi MAMA ISMAIL anadai kuwa kijana huyo siomgeni katika macho yake na alikuwa wameishi pamoja kule Mwanza katika Kota za Polisi ambapo wazazi wao walikuwa watumishi wa serikali takribani miaka 10 iliyopita. MAMA ISMAIL amebainisha siku ya tukio walistukia kijana huyo amelala Barazani akionekana amechoka na mchafu kutokana na kuona hilo wakaamua kumuwekea mlinzi maalum wakazi wote wa eneo hilo na kuamua kulala nae nje lakini hata hivyo walinzi hao walizidiwa na kujikuta wamepitiwa na usingizi. Na ndipo mara MAMA ISMAIL akashangaa kumuona mtu ambaye walimuacha nje tayari akiwa ndani ilihali milango na madirisha ikiwa imefungwa na alipoulizwa ameingiajeingiaje alijibu kwa kuonyesha herufi ambazo aliziandika chini na kuonyesha jinsi gani alivyoweza kuingia kimgongomgongo bila kikwazo chochote. Na alipoulizwa ni kitu gani kimemleta alibainisha kuwa ametumwa na mama yake kumchukua ISMAIL, na amebainisha katika safari yake alikuwa ameambatana na wenzie na jumla walikuwa watano, lakini wenzie wameishia eneo la UBENA,Morogoro na yeye kuamua kuja Kongowe. Mpaka sasa mtu huyo anashikiliwa katika kituo cha Polisi cha Tumbi kwa mahojiano zaidi, ili kujua zaidi kuhusu mtu huyo ambaye ujio wake umewashangaza wengi na jinsi alivyokuwa na uwezo huo unaosadikiwa kuwa ni wa kishirikina. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA