KANISA LAWASAIDIA WALEMAVU.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/26-May-13/9:55:05
Makanisa nchini yametakiwa kuwajenga waumini wao kwa misingi ya kuheshimu haki na amani ili kuweza kutoa fursa kwa waumini kuabudu wanachoamini kutokana na hali utulivu iliyopo kutokana na misingi imara iliyoachwa na viongozi wa mwanzo.
Akizungumza katika harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kununua kiwanja cha kanisa hilo la PENTECOSTAL MISSIONARY CHURCH kutokana na kwa sasa kuwa katika eneo la hifadhi ya barabara ya kuu ya Morogoro, Mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa ya CCM mkoa wa Pwani BW. RUGEMALIRA RUTATINA amesema kanisa linawajibu wa kukemea na kutoa maelekezo kwa serikali kuhusiana na suala zima la kutunza amani iliyopo.
BW. RUTATINA amesema Taasisi za dini zimekuwa zinaisaidia serikali katika kuhakikisha amani iliyopo inadumu bila kuvurugwa, na serikali katika hilo imekuwa ikiunga mkono juhudi hizo zinazoonyeshwa na kanisa katika kuhakikisha nchi inakuwa na ustawi.
Mchungaji GERVAS MASANJA amesema Kanisa lao katika kutambua nia ya serikali ya kuletea maendeleo wananchi wake imeazimia kufanya upanuzi wa Barabara ya Morogoro, na kwa kuliona hilo na faida yake kwa jamii wao kama taasisi ya kiimani imeamua kutafuta eneo jingine kwa ajili ya ujenzi wa kanisa jipya na hali imewafanya kuandaa harambee za kuwezesha upatikanaji wa kiwanja na ujenzi.
Mchungaji MASANJA amesema mpaka sasa wameshapokea michango kutoka kwa wadau mbalimbali ikiwa pamoja na makanisa yaliyopo mjini Kibaha, watu binafsi na viongozi mbalimbali, mbali ya kuendesha zoezi hilo lililoshuhudiwa na Diwani wa Pangani, BIBI. MWANAID KIONGOLI, Mjumbe wahalmashauri kuu ya chama cha mapinduzi, BW.RUGE alikabidhiwa baiskeli maalum za wenye ulemavu kwa walengwa.
Baiskeli hizo nimiongoni mwa Baiskeli 12 za watu wenye ulemavu zilizotolewa, ambapo nane kati ya hizo zimetolewa kwa kituo cha afya mkoani na Hospitali teule ya Tumbi kila moja baiskeli nne.
END.
Comments
Post a Comment