KINAMAMA WAPATIWA MSAADA WA PAMPU

Ben Komba/Pwani-Tanzania/10-May-13/19:33:06 Mlezi wa Jumuiya ya kinamama wa CCM mjini Kibaha ametoa msaada wa pampu ya kumwagilia maji kwa akinamama kutoka katika Kata ya Tumbi yenye thamani ya shilingi laki tano na kumi elfu kwa ajili yakuwasaidia katika shughuli zao za kilimo na kujipatia kipato. Akikabidhi pampu hiyo kwa akinamama hao, Mlezi wa UWT BIBI.SELINA KOKA ambaye pia ni Mke wa mbunge wa Kibaha mjini, BW. SYLVESTER KOKA amesema kuwa hatua hiyo kuwasaidia kinamama hao kitendea kazi hicho kufuatia ahadi aliyowapa kinamama hao siku ya maadhimisho ya siku ya wanawake ulimwenguni. BIBI.KOKA amebainisha kwamba anaamini kwa kuwasidia kinamama hao kutawawezesha kupunguza umaskini kwa njia moja au nyingine toka kikundi chao kinafanya shughuli za ukulima wa mboga mboga, na kwa kuwapatia kifaa hicho uzalishaji wa mboga utaboreka na kuwa rahisi kutokana na kupata nyenzo hiyo. Akizungumzia kuhusiana na soko la mbogamboga ambazo kikundi hicho cha kinamama kata ya Tumbi kitazalisha, BINBI.KOKA amewahakikishia soko la uhakika kina mama hao pamoja na kinamama wote ambao wanajishughulisha na ukulima wa mboga mboga kuwa kutakua na gari maalum ambalo litakuwa linapita kuanzia Ruvu kukusanya mbogamboga kwa ajili ya matumizi ya hoteli yake. amefafanua kuwa madhumuni makubwaya kufanya hivyo ni kuhakikisha anatoa fursa kwa kinamama kuweza kujiajiri katika suala zima la utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi katika kuwajengea uwezo wa kiuchumi kwa akinamama ambao wana nia ya kweli ya kujiajiri. Mmoja wa akinamama waliokabidhiwa pampu hiyo kwa ajili ya matumizi ya kilimo cha umwagiliaji, BIBI. MAIMUNA SALUM amemshukuru Mama KOKA kwa kitendo chake cha kutimiza ahadi yake aliyotoa wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake ulimwenguni, na kumuomba MUNGU ampe uhai wake ili aweze kusaidia watu wengine wenye huhitaji. Akizungumza katika hafla hiyo katibu wa CCM mjini Kibaha, BIBI. MWAJUMA NYAMKA amempongeza BIBI. SELINA KOKA kwa kutupia macho kinamama wenzie na kuwasaidia katika masuala muhimu ya kuwainua kutoka katika hali dhaifu na kuweza kujimiliki kiuchumi. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA