CCM WATISHA MJINI KIBAHA MWISHONI MWA WIKI.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/12-May-13/9:49 PM Vijana wa chama cha mapinduzi mkoa wa Pwani wametakiwa kuwa kitu kimoja katika kuhakikisha wanaimarisha umoja na mshikamano katika Chama chao na kuepuka mifarakano isiyo ya lazima. Akiongea katika ziara yake kuzungukia Kata 11 zilizopo mjini Kibaha Mwenyekiti wa CCM, BW. IDD KANYALU kwa lengo la kutoa shukrani kwa wanachama wa chama hicho ambao walimpigia kura wakati wa uchaguzi wa ndani wa chama hicho. BW. KANYALU amesema akiwa kata ya Mailimoja katika kipindi cha uchaguzi kulikuwa kuna changamoto mbalimbali ambazo zimejitokeza kiasi cha kuzua makundi ambayo hayawezi kukisaidia chama kwa namna yoyote ile. BW. KANYALU amebainisha kuwa kwa sasa ni vyema kwa vijana kusahau tofauti zao za kipindi cha uchaguzi ili kuweza kutekeleza majukumu yao kwa umakini wa hali ya juu na kukipatia chama mafanikio. Akiongea katika mkutano huo katika kata ya Mailimoja, Mwenyekiti wa chipukizi Kata ya Mailimoja, Binti mdogo IMRAN MOHAMED amesema kwa upande wake anachojua kuwa katika umoja wa vijana na Chipukizi hakuna tatizo, bali matatizo yapo ndani ya chama chenyewe na amewataka wavunje makundi maramoja. Katika hatua nyingine Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM, BW. RUGEMALILA RUTATINA amefungua shina la wakereketwa la MTAZAMO lililopo katika kata ya Tumbi na kuwasihi kushirikiana na chama hicho katika mambo mbalimbali. BW. RUTATINA amesema hatua ya Vijana wa hapo kuanzisha shina hilo ni kutoa fursa kwao kuweza kushauri aqu kuchangia mawazo yao katika kukimarisha chama cha Mapinduzi. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA