WANAWAKE VIJANA HURU NA MAENDELEO.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/10-Mar-13/18:48:18
Mpango wa wanawake vijana uhuru na maendeleo unaoendeshwa kwa pamoja kati ya ACTION AID na shirika lisilo la kiserikali la YOUTH PARTNERSHIP COUNTRYWIDE -YPC- lenye maskani yake mjini Kibaha limefanikiwa kuwafikia walengwa takriban 400 katika suala zima la kuwapatia wanawake hao vijana elimu juu ya kujitambua na ujasiriamali.
Mratibu wa mpango kutoka YPC, BIBI. GROLIA MABERE amesema mpango huo unanuia kuwafikia wanawake vijana 2000 nchi nzima, kwa wilaya ya Kibaha mradi huo umegusa katika halmashauri zote mbili ya mjini na kijijini, kwa kuwakusanya wanawake kutoka katika kata mbalimbali na kuwasaidia kuunda vikundi na kufanya uchaguzi wa viongozi wao.
BIBI. MABERE amebainisha kuwa mpaka sasa wamefanikiwa kuwaamsha wanawake vijana na kujitambua na kuweza kushiriki katika mambo mbalimbali ya kitaifa na mtaa ikiwa pamoja na kushiriki chaguzi mbalimbali zinazojitokeza katika maeneo yao.
Mratibu huyo wa mpango wa wanawake vijana kutoka YPC, BIBI. GROLIA MABERE ameongeza mbali na elimu ya ushawishi na utetezi ambayo ina lengo la kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele katika kupambana na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto na wanawake.
Mbali ya elimu hizo wanawake vijana hao wanapatiwa pia elimu ya ujasiriamali ili kuwawezesha waweze kujitegemea kiuchumi kwa kupatiwa mbinu stahili ambazo kama wakizitumia ipasavyo kama ilivyojidhihirisha kwa baadhi ya wenzao nwengine ambao wametumia elimu hiyo ambayo wameipata kuzalisha bidhaa mbalimbali ambazo zinawasaidia kuwaingizia kipato.
Naye Mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la YPC, BW. ISRAEL ILUNDE amesema kwa kipindi cha miaka miwili shirika lao limekuwa likiendesha mpango huo wa kuwakomboa wanawake vijana kutoka katika kiza kinene na kuwapatia mwanga ambao umewawezesha kujifunza masuala yanayohusiana na elimu ya uraia, ushawishi na utetezi katika kuhakikisha wenyewe wanakuwa na nguvu ya kusimamia haki zao.
END.
Comments
Post a Comment