POLISI JAMII NA ELIMU MAALUM

Ben Komba/Pwani-Tanzania/11-Mar-13/20:05:34 Jeshi la Polisi nchini linafanya utafiti maalu yenye lengo la kujua mafanikio yaliyopatikana katika sera yake ya Polisi Jamii ambayo imelenga kuishirikisha jamii kikamilifu katika suala zima la ulinzi na usalama wa watu na mali zao. Katika utafiti huo ambao ulihusisha makundi ya watu tofauti katika jamii kwa kuwapatia madodoso yenye maswali ambayo washiriki walitakiwa kujaza kwa kadiri ya maono yao kuhusiana na utendaji wa Jeshi la Polisi katika suala zima la Polisi jamii katika kuhakikisha kunakuwepo na kuaminiana kati ya wanajamii na Polisi. Nikiongea na Mratibu msaidizi wautafiti huo katika mkoa wa Pwani, INSPEKTA ATHUMAN MTASHA amesema utafiti huo katika Mkoa wa Pwani utahusisha wilaya za Kibaha na Mkuranga na makundi mbali yameshafikiwa yakiwemo waandishi wa habari, walimu, watendaji na wafanyakazi wa kada mbalimbali. Naye mmoja wa watafiti wasaidizi amesema wao wanatekeleza agizo kutoka Jeshi la Polisi Tanzania na wao wametoka katika Chuo kikuu cha Dar es Saalam ili kushirikiana na Jeshi la Polisi kutekeleza zoezi hilo ambalo amesema linafanyika kufuatana na kanda, na linafanyika nchi nzima kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wa Jeshi hilo na ripoti itakapokamilika itawasilishwa kwa IGP, SAID MWEMA. END. Ben Komba/Pwani-Tanzania/07-Mar-13/08:53:24 PM Walimu wa elimu maalumu wameitaka serikali kutoa mafunzo na nyenzo kwa walimu wanaojihusisha na kuwafunza watoto wenye ulemavu mbalimbali ili kuwawezesha kuelewa masomo ili yaweze kuwasaidia katika maisha yao ya baadaye. Mwandishi wa habari hizi hivi karibuni amebahatika kukutana na mwalimu wa elimu maalum, MWL. ANNA LULANDALA ambaye amebainisha kuwa wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa pamoja na Walimu hao kuwajibika kusimamia wanafunzi wote wenye ulemavu bila kubobea kuhudumia watoto wa aina fulani tu ya ulemavu katika kuwarahisishia walimu kutumia elimu yao kwa weledi. MWL.LULANDALA amebainisha ingekuwa vyema kwa walimu wa elimu maalum kugawika kwa kadiri ya aina ya ulemavu badala ya walimu kuwajibika kuwahudumia kwa ujumla wao, hali ambayo inafanya mazingira ya utoaji wa elimu hiyo kuwa magumu, kutokana na walimu kuchanganyikiwa kwani mara yupo na mtoto mwenye mtindio wa ubongo akitoka hapo anakumbana na mtoto mwenye ulemavu wa kusikia hivyo hali hiyo inawapa wakati mgumu walimu wanaotoa elimu hiyo kwa watoto wenye ulemavu. Mbali ya changamoto hizo kumekuwepo na tatizo kubwa la nyenzo wezeshi kwa walemavu wa kusikia ambao wanahitaji kuwa na vifaa maalum ya kuwawezesha japo kusikia kidogo, ukosefu wa kofia, miwani na mafuta maalum kwa maalbino nalo ni tatizo, hivyo amewaasa wananchi, taasisi binafsi na serikjali kuwasaidia watoto walemavu ili waweze kupata elimu stahili. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA