BARABARA ZACHONGWA MJINI KIBAHA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/10-Mar-13/20:04:51 Halmashauri ya mji wa Kibaha imeendelea na mpango wake wa kuhakikisha barabara katika halmashauri ya mji wa Kibaha zinachoingwa na kuziweka katika hali nzuri ya kupitika katika kipindi cha chote cha mwaka, hali hiyo imekuja kufuatia halmashauri hiyo kuwa na Greda ambalo kwa njia moja au nyingine linarahisisha baadhi ya shughuli za ujenzi katika katika halmashauri. Mhandisi wa ujenzi halmashauri ya mji wa Kibaha, BW. EZEKIEL KUNYARANYARA amesema lengo ni kuchonga barabara zote ambazo zipo kisheria katika kuhakikisha usumbufu unapungua kwa watumiaji na kusaidia katika kuweza kupanga mji katika mpangilio unaoeleweka kwa kuimarisha miundo mbinu ya barabara. Mhandisi KUNYARANYARA amesema barabara zote hizo kwa kuanzi zitakuwa katika kiwango cha udongo, wakati halmashauri ikijiandaa na mikakati mingine ya baadaye ikizingatia upatikanaji wa fedha ambazo itasaidia kuimarisha miundombinu ya barabara katika mji wa Kibaha kama alivyokutwa na kamera ya Mwandishi wetu akiwa eneo la kazi akisimamia kazi hiyo katika maeneo ya ofisi mjini Kibaha. Aidha Mhandisi KUNYARANYARA amesema kuwa katika zoezi hilo wamekuwa wakikabiliana na changamoto mbalimbali kama kukata wakati mwingine kwa bahati mbaya mabomba yanayosambaza maji baadhi ya maeneo na jambo jingine ambalo ni changamoto ya haja ni baadhi ya wananchi kujenga katika maeneo ya barabara. Mji wa Kibaha ni majuzi tu umepata barabara baada ya miaka mingi ya kuwa na barabara ya vumbi pamoja na kutolewa fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami katika vipini tofauti bila mafanikio na hatimaye mwishoni mwa mwaka jana chini ya Mbunge wa Chama cha Mapinduzi, BW. SYLVESTER KOKA ambaye moja ya ahadi zake wakati wa kampeni ya uchaguzi uliopita alisema kuwa atahakikisha Mji wa Kibaha unakuwa na barabara ya lami. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA

MAMLAK YA MJI MDOGO MLANDIZI HOI.

VIDEO - CWT WACHAGUANA PWANI.