SIKU YA WANAWAKE

Ben Komba/Pwani-Tanzania/10-Mar-13/10:29:44 Mkuu wa mkoa wa Pwani, BIBI. MWANTUM MAHIZA amewakumbusha wanawake kuhusiana na wajibu walio nao kama walezi kuutekeleza kikamilifu katika kuliletea Taifa ustawi wa kimaadili kwa familia zao na kuimarisha Amani ya taifa. BIBI. MAHIZA amesema wanawake watambue kuwa wao ni walezi wa watoto wao na watoto wa wanawake wenzao na vilevile wanawajibu wa kulea watu walio karibu nao na amewataka kutosita katika kushauri kwa ajili ya mustakabali mzuri wa taifa ambao utalenga katika kuimarisha amani ya familia na kuchochea maendeleo ya kijamii. BIBI. MAHIZA amewataka wanawake kukumbuka msemo unaosema NYUMA YA MWANAUME MWENYE MAFANIKIO KUNA MWANAMKE MWEREVU ambaye kwa njia moja au nyingine anamuwezesha mwanamume wake katika mambo mbalimbali ambayo yanasaidia kumjenga kiakili na kiafya na kumuwezesha mume kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Akizungumza katika Hafla aliyoiaandaa kwa ajili ya siku ya wanawake Duniani, Mke wa Mbunge wa Kibaha, BIBI. SELINA KOKA amewashukuru viongozi na wanawake waliojitokeza kwa wingi kutoka kata mbalimbali za mjini Kibaha kwa kukubali kufika na kusheherekea siku hiyo kwa pamoja. Awali katika tukio lililoambatana na siku ya wanawake ulimwenguni kina mama mjini Kibaha wametoa msaada kwa wagonjwa ambao wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa ya Tumbi, ambapo wameweza kuwapatia wagonjhwa hao maji, juisi, dawa za mswaki, kandambili. Mmoja wa kinamama mama hao BIBI. ELINA MGONJA amesema wameamua kufanya hivyo mwka huu katika maadhimisho ya siku ya wanawake ni kutaka kuonyesha kuguswa kwao na mahitaji mbalimbali wanayohitaji wagonjwa na hasa ikizingatiwa kutokana na hali yao hawawezi kufanya shughuli ya kujiingizia kipato na hivyo kuhitaji msaada wa hali na mali kutoka wenye uzima wa afya. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA