WABUNGE WAHITIMU MAFUNZO 832 KJ.

WABUNGE WAHITIMU MAFUNZO 832 KJ. Ben Komba/Pwani-Tanzania/29-Mar-13/09:46:30 Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, DKT. JAKAYA KIKWETE amekumbuka ujasiri ambao aliupata kutokana na yeye kupitia Jeshi la kujenga Taifa kwa mujibu wa sheria,akiwa katika kombania C ambapo alikutana na watu mbalimbali na kupata uzoefu mkubwa wa kimaisha. DKT. KIKWETE amebainisha kutokna na kupitia kwa mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa kwa mujibu wa sheria na kubahatika kupangiwa katika kikosi cha 832 cha Jeshi la kujenga Taifa Ruvu, na amewapongeza wabunge ambao wamehitimu mafunzo yao ya wiki tatu kwa kuonyesha uzalendo. Katika ziara hiyo Rais huyo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu, DKT. JAKAYA KIKWETE ametembelea maeneo mbalimbali ya miradi ya kikosi na kuona nyumba namabweni ya vijana wa JKT na kufunga mafunzo maalum ya JKT kwa wabunge ambao wamehudhuria mafunzo hayo ambayo yalianza March 4. Wabunge ambao wamehudhuria mafunzo hayo ni, BW.DAVID SILINDE, BW. MURTAZA MANGUNGU, BW.LIVINGSTONE LUSINDE, BW.YUSUPH KHAMIS, BW.SAID MTANDA, BW.MENDRAD KIGOLA, BW.NEEMA HAMID, BI. HALIMA MDEE na ESTHER BULAYA ambao wamehitimu mafunzo hayo katika kambi ya Ruvu. Akisoma taarifa ya wabungea ambao wamehudhuria mafunzo hayo katika kikosi cha kujenga Taifa Ruvu 832 KJ, Mbunge wa viti maalumu BI. EASTHER BULAYA ameishauri serikali kuongeza muda wa mafunzo hayo kwa vijana ambao wataingizwa kwa mujibu wa sheria na kujitolea ili kuweza kuwajenga kikamilifu kiakili na kimwili katika suala zima kujenga uzalendo. BI. BULAYA ameongeza kuwa na itakuwa vizuri kama serikali ikatengeneza maingira mazuri kwa viajana wanaomaliza mafunzo hayo kwa lengo la kutowaacha bila kazi ya kufanya mara watakapomaliza mafunzo hayo na hasa ikizingatiwa mafunzo hayo yanawawezesha kutmia silaha za aina mbalimbali ikiwa pamoja na kupatiwa mbinu za medani ambazo kama zikitumiwa vibaya zinaweza kuja kusababisha maafa kwa Taifa. Baada ya hapo Rais KIKWETE alipata fursa ya kufungua mafunzo hayo ya miezi mitatu kwa mujibu wa shertia kwa kufyatua risasi angani kwa kutumia bastola maalum inayotumika kuashiria mambo mbalimbali vitani kama ishara ya kufungua rasmi mafunzo hayo. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA