MGOGOROWA ARDHI

Ben Komba/Pwani-Tanzania/23-Mar-13/08:51:18 AM Wakazi na wakulima wa vitongoji vya Kisabi na Kiwalani katika halmashauri ya wilaya ya Kibaha wameazimia kuifikisha halmashauri hiyo mahakamani kuhusiana na hatua ya idara ya ardhi kupima maeneo yao na kuweka mawe kuonyesha kuwa viwanja hivyo vimepimwa bila kuwashirikisha. Nikiongea na Katibu wa Jumuiya ya wakulima na wakazi wanaokaa katika vitongoji hivyo BW. ABILAHI SAAD amebainisha kuwa wao kwa pamoja wamekutana na kuazimia kulifikisha suala hili mahakamani kwa lengo la kupatiwa ufumbuzi wa kisheria. BW. SAAD amefafanua kuwa kuna fununu kwamba eneo hilo linataka kutolewa kwa wafanyabiashara ambao wanqapata nguvu kutoka halmashauri kana kwamba wao ni weageni katika nchi na huku kuweepo kwa mji wa Mlandizi ni kuwepo kwa watu wanaoishi eneo hilo, hivyo amelaani tabia ya watendaji wanaotokla maeneo mengine kupuuza haki za wazawa wa maeneo wanayofanyia kazi. Amewataka watendaji kabla ya kufanya maamuzi makubwa kama ya kumnyang'anya mtu ardhi yake bila kumshirikisha kwa malengo yoyote hata kwa lengo la kuiongezea halmashauri kipato, kwanza kuzingatia historia ya eneo husika na kuheshimu uwepo wao kama ilivyo katika eneo hil ambalo linaaaa nyumba zime4jengwa zaidi 50 na kujaribu kuwahamisha ni kuwababishia usumbufu usio wa lazima kwa maslahi ya watu wachache. Naye Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha, BW. ANDO MWAKIBUGA amesema anachofahamu yeye kuwa vikao vya kisheria vimekaa na miniti za mkutano zipo na vikao vya wananchi vimefanyika kabla ya kuanza utekelezaji wa mpango huo wa upimaji wa viwanja. BW. MWAKIBUGA amesema kuwa taarifa ambazo alizipata yeye ni kuwa Mkurugenzi wa halmashauri ya Kibaha na Mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari Ruvu wanataka kupora maeneo ya Ruvu Kisabi, lakini anashangaa kusikia madai ya kuwa wananchi hawakushirikishwa wakati inaonekana wamehudhuria na kujioredhesha kwenye vikao mbalimbali vilivyoifanyika katika kukubaliana kutoa eneo hilo kwa mwekezaji. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA