MGOGORO STENDI
Ben Komba/Pwani-Tanzania/27-May-13/19:42:08
Sakata kubwa limeibuka kufuatia amri ya kuwataka wafanyabiashara wanaotoa huduma ya kutoa na kupokea fedha kwa njia ya simu za mkononi sawa na wauza vocha na wafanyabiashara wengine kuondoa vibanda vyao vya biashara katika eneo hilo.
Kamera ya SIBUKA TV imeshuhudia wafanyabiashara hao wakimsongasonga mmoja wa wanamgambo wa halmashauri ya mji kwa kiklichodaiwa kupita na kuandika vibanda vyao kutumia rangi ya mafuta ya kupuliza neno ondoka hali iliyozua ghadhabu kiasi cha kukaribia kumuadhibu mgambo huyo.
Mazingira ya watu wanaofanya shughuli zao kutokubaliana hatua ya Mgambo hao kupita wakiandika kila kitu kilicho mbele yao, ONDOA hali iliyozua taharuki miongoni mwa wafanyabiashara hao ambao wanadai wanafuata taratibu zote za kisheria kuwepo katika eneo hilo.
Akiongea kuhusu tujkio hilo la mgambo wa halmashauri kupita kuandika katika maeneo mbalimbali ya vibandavya stendi, Bwana afya wa Kata ya Mailimoja, BW. ABUBAKAR SHAH amesema wao wanachofanya ni kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Afisa afya wa mji, na kusema wao hawatarudi nyuma mpaka wamehakikisha wametekeleza maagizo waliyopewa.
Diwani wa Kata ya Mailimoja, BW. ANDREW LUGANO amesema yeye binafsi amekwenda kumuona Mkurugenzi akiambatana na Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mailimoja ili kujua ni nani ambaye ametoa agizo la kuondolewa kwa vibanda vile ambavyo ndio kwa kiasi fulani ni mhimili wa kiuchumi wa wananchi wa kawaida katika sulal zima la kutuma na kupokea fedha.
Diwani LUGANO amebainisha kuwa alipofika kule Mkurugenzi amekana kuhusika na zoezi hilo, na kuahidi kulifuatilia kujua taarifa sahihi.
END
Comments
Post a Comment