UONGOZI WA ZIMAMOTO WAKABIDHIWA ZAWADI.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/Monday, 06 May, 2013/06:58:25 PM Uongozi wa Kikosi cha uokoaji na zimamoto katika Mkoa wa Pwani umekabidhiwa rasmi zawadi ya mshindi tatu ya Kombe la SUPER CUP michuano yake iliyomalizika hivi karibuni,   Akikabidhi zawadi hiyo kwa Kaimu Kamanda wa Kikosi cha uokoaji nazimamot Pwani, Kamishna msaidizi JUMA ATHUMAN YANGE, Mwenyekiti wa timuya FIRE FC, BW. RICH KIBAJA amebainisha kuwa wamefanya hivyo kutpokana na mchango mkubwa unaotolewa na Kikosi cha zimamoto na uokoaji kwa timu hiyo.   Aidha Kibaja amekiomba kikosi hicho kukipanua kiwanja chao cha mazoezi ili kutoa fursa ya kuwepo angalau kiwanja kimoja chenye vipimo stahili kwa ajili ya kutumika kwa michezo mbalimbali tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo hakuna kiwanja chamichezochenye sifa mjini Kibaha.   Akipokea zawadi hiyo ya jezi seti moja waliyopata timu hiyo ya FIRE FC, Kaimu Kamanda wa Kikosi cha uokoaji na zimamoto Kamishna msaidizi JUMA ATHUMAN YANGE amewapongeza wachezaji kwa jitihada walizoonyesha na kufanikiwa kupata zawadi hiyo ya mshindi wa tatu, ingawa lengo ilikuwa kuwa washindi wa kwanza.   Kamishna msaidizi YANGE amesema kwa upande wao wataendelea kushirikiana na vijana wanaocheza katika mambo mbalimbali na kipaumbele ikiwa ni kiwanja cha mpira kusawazishwa na kwa kushirikiana na wataalam wengine ili kuweza kupata vipimo sahihi vya kiwanja cha mpira na ikiwezekana na michezo mingine. END.  

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA